?Vitu vizuri mara nyingi hua vinakuja wakati haupo tayari. Utayari unautengeneza wewe mwenyewe.
➿Wengi bila kujua huishia kujitetea na kutoa sababu nyingi za namna ambavyo hawawezi na kujikuta wakipoteza fursa zile au vitu vile.
✅Choose to find a way don’t find an excuse!
? Unaweza ukajitetea sana jinsi ambavyo hali ni ngumu.
?Unaweza ukajitetea sana jinsi ambavyo huwezi kufikia malengo na ndoto zako lakini ukweli unabaki kwamba hizo sababu na kujitetea hakukubadilishii hali uliyonayo.
? Uchumi umekua mgumu sana unaweza kutumia hiyo kama sababu ya kujitetea au kama fursa ya kutafuta suluhisho.
☹ Hata Mungu hataki watu wanaojitetea na kutoa sababu kwanini hawawezi na kwanini wamekosea. Kaa kwenye nafasi yako utatue matatizo yako.
?Ifanye akili yako ifikiri. Akili ikishindwa kutumika vyema itatumika vibaya.
#Jacob_Mushi
#+255654726668