Aliwahi kusema Charlie Jones kwamba utakuwa mtu yule yule miaka mitano ijayo isipokuwa watu utakaokutana nao na vitabu utakavyosoma. Hii ina maana kwamba kama utaendelea kubaki na vitu vile vile ambavyo umekuwa unavifanya utaendelea kubaki vile vile. Hii pia ina maana kwamba maisha yako ya sasa ni mchango wa watu ambao umekutana nao miaka 5 iliyopita na vitabu au maarifa ambayo uliyapata miaka 5 iliyopita.

“You will be the same person in five years as you are today except for the people you meet and the books you read.”
― Charlie Tremendous Jones

Ukweli ambao ulikuwa huujui ni kwamba maisha uliyonayo ni matokeo ya juhudi ambazo umekuwa unaweza miaka michache iliyopita. Yatazame ni aina gani ya maisha unayoishi sasa, zitazame juhudi ulizoweka miaka michache iliyopita. Kama juhudi ndio zile zile unaendelea nazo mpaka sasa maana yake maisha yako yataendelea kuwa hivyo yalivyo au yatazidi kupungua ubora.

Juhudi hizo zinaweza kuwa ni katika kusoma vitabu, kujiendeleza, kutafuta pesa kwa bidii, kuendelea kutegemea kazi ile ile ambayo uko nayo na juhudi nyinginezo.

kama umeshajua hivyo rafiki kwanini sasa unataka kuendelea kubaki hivyo ulivyo sasa? Umeshaweka mpango wa kubadili maisha yako? Umeshaweka mpango wa kuongeza maarifa na watu wengine ambao watakuinua Zaidi?

Maisha yako ni Jukumu Lako, hakuna mtu mwingine anayajali sana maisha yako kuliko wewe mwenyewe. Nilikwambia pia kwenye Makala iliyopita hakuna anaekulazimisha, wewe mwenyewe ndiye utakaeamua kuchukua hatua au kusoma na kuacha hiki ulichokisoma.

Pamoja na hayo nataka nikuulize je katika miaka 5 iliyopita kuna kitu ambacho umekuwa unasumbuka sana kukibadili kwenye maisha yako? Kama kipo basi napenda kuwa rafiki yako mpya katika kukusaidia kwenye kitu hicho. Ili uweze kuwa karibu nami bonyeza link hii hapa ufuate maelekezo >>> https://jacobmushi.com/kocha/

Naomba Nikuache na Msemo Huu >>>

“Usiwachukulie Poa Wale Waliokutia Moyo Kipindi Hakuna Anaekujua kwasababu Hawa ndio Waliojua Ile Mbegu Ilikuwa Ndani Yako” -Jacob Mushi.

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading