532; Uliza.

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Shida kubwa tuliyonayo watu wengi ni kujipa majibu ya maswali ambayo tunajiuliza wenyewe kuhusu watu wengine. Mara tu unapoingiwa na wasiwasi kichwani mwako juu ya jambo fulani usiishie kujipa majibu mara nyingi utajikuta unajipa majibu ya uongo.

Unapojikuta kwenye wasiwasi wa jambo fulani ndani ya akili yako usikubali kujipa majibu mwenyewe ULIZA SWALI. Unapouliza ndio utaweza kujua ukweli au kufahamu kwa upana zaidi juu ya kile ulichokuwa unajiuliza mwenyewe.

Unapouliza wengine utakutana na mitazamo tofauti ambayo wengine nao huwa nayo na itakusaidia katika zile fikra ulizokuwa nazo mwenyewe. Usikubali kujipa majibu mwenyewe kwasababu unaweza kujidanganya na mwisho wa siku ukafanya maamuzi ambayo sio sahihi.

Kuna sehemu nyingi za kuuliza maswali yanayokusumbua. Unaweza kuuliza kwenye mtandao wa Google, unaweza kumuuliza mshauri wa maswala ambayo yanakusumbua, unaweza kuumuliza mtu mzima ambaye ameshapitia kile unachokipitia, unaweza kuumuliza moja kwa moja kama ni mtu ambaye anakupa wasiwasi juu ya jambo fulani.

Mara nyingi majibu utakayojipa mwenyewe yanaweza yasiwe sahihi kwasababu yataendana na mtazamo wako ulivyo juu ya kile kitu kinachokutatiza. Unapowauliza wengine utapata majibu ya tofauti kwasababu kuna watu wenye viwango vya juu zaidi katika kile kinachokutatiza.

Bahati nzuri sana kama umeweza kusoma makala hii tayari umeshapata mtu wa kumuuliza yale yanayokutatiza. Unaweza kuniuliza chochote ambacho kinakupa mawazo na wasiwasi. Usikubali kabisa kuishia kujipa majibu na mwisho wake ukajikuta umefanya makosa makubwa kwenye maisha yako.

Karibu sana Uniulize Swali juu ya changamoto, wasiwasi, na tatizo lolote linalokutatiza. Njia rahisi ya wewe kuniuliza swali ni kuwa na mawasiliano yangu ya simu (WhatsApp) na mimi nitakupa utaratibu mzima pale unapokuwa na jambo linalokutatiza.

Kupata Mawasiliano yangu Bofya Maneno Haya

Kupata vitabu vya kukupa maarifa na kukuwezesha kushinda Bofya Hapa

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
4 Comments

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading