Watu wanaweza kukuchukia pasipo na sababu yoyote ya msingi.
Inawezekana hata hujawahi kuwasemesha lakini wakakuchukia.
Inawezekana hujawawahi kuwatendea jambo lolote lile baya au la kuudhi lakini wakakuchukia tu.
Unapaswa tu kutambua kwamba hata ufanye mambo mema kiasi gani hapa duniani huwezi kupendwa na kila mtu.
Huwezi kumridhisha kila mtu.
Unaweza kuzungumza sentensi moja ikamsaidia mtu mmoja, na mwingine akaona unamsema vibaya.
Endelea Kufanya Kile Ulichokuja kufanya Hapa Duniani na uwe tu unaelewa kwamba HUWEZI KUMRIDHISHA KILA MTU.
Jacob Mushi.