ACHA KUJIFARIJI

By | July 16, 2016
Kuna watu hujifariji kua “Mungu ndie ajuae kesho.”

Ukweli ni kwamba Mungu sio kesho tu anajua yeye anajua kila kitu hata mwisho. Hata ugonjwa utakao kupata mwezi ujao kwa ulaji mbovu wa leo anajua.

Kua na maono, malengo na mipango fanyia kazi kila siku Mungu atakulinda na mabaya yote kutokana na kile unachokifanya.

Kama huna maono unafikiri Mungu atakuwekea ulinzi wa faida gani?

“Eti Tunapanga tu lakini Mungu ndie anaejua yote”

 Ni kweli alijua pia utazaliwa kabla hujazaliwa.
Na amekuacha hai hadi sasa ili angalau uone mbele.

Kama vitu vyote unavyovifanya wanyama wengine wanaweza kufanya pia una hatari ya kuondoka duniani.

 “Kuzaa, Kula, Kulala, Starehe “

Nenda nje ya hapo onyesha uwezo wa tofauti na wanyama wengine.

#JacobInspirationalTeachings2016
#Contact: 0654726668

Leave a Reply