Natamka baraka katika kila unalokwenda kulifanya week hii. Matokeo makubwa zaidi katika kila unalolifanya.

Inawezekana umepitia ugumu sana kwenye mambo mengine na wakati mwingine ukataka kukata tamaa.  Week hii ni ya kwako wewe kwenda kufungua kila lilokwama.

Hakuna lisilowezekana pale unapokua na imani.  Imani yako ndio itakuwezesha wewe upate chochote unachotaka.

Lakini baada ya kua na imani kubwa kinachofuata ni matendo. Lazima matendo yako yawe makubwa.

Ongeza nguvu kubwa na maarifa zaidi kwenye matendo ukibakia kwenye imani huwezi kuona matokeo yeyote.  Anza leo kufanya vitendo zaidi na utakapopata matokeo imani yako itaongezeka zaidi.

Hii pia ni week ambayo tunakwenda kukamilisha nusu ya mwaka wetu huu 2016. Ni week ya kujitathimini. Kwenye kila lengo ulilojiwekea mwaka huu jipime uone umefikia wapi na unaelekea wapi. Kama upo pale pale ni tatizo linalohitaji suluhisho.

Nikutakie wiki yenye baraka tele na matokeo ya matendo ya imani yako.

Mwandishi: Jacob Mushi
Email: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading