512; Mimi Ni Mtenda Dhambi Kuliko Wewe.

Siku Moja nilikuwa nawaza hivi, “Siku Nikifa Nikakuta hakuna Mungu Nitacheka Sana”, Sauti nyingine ndani yako Ikasema, “Hapo Utakapokuwa Unachekea ni Nani Huyo Atakuwa Amekutengenezea” Ndugu Yangu Mungu Yupo, Ukatae Ukubali………………… Kuna ule mtazamo wa kuwaona watu ambao wamefanya mambo makubwa, na wale wenye ushawishi mkubwa sana kuwa hao ni watu wasio na makossa kabisa. […]

511; Unakimbilia Wapi? Tazama Pembeni Yako.

 Haya Ndio Maisha yetu kwenye vitu vingi tunavyopitia kila siku, Soma kisa hiki ujifunze: “Habari kaka Jacob, ninaomba ushauri wako kuhusu hili. Ni mwaka wa tatu sasa tangu nikutane na binti mmoja na nikampenda sana. Nina tabia moja huwa sikati tamaa haswa pale ninapokuwa nimekipenda kitu Fulani maishani mwangu. Nimekuwa naamini kwamba ipo siku tu […]

510; Ninajihisi Kama Mtu Aliekwama Kwenye Tope.

“Kaka Jacob naomba ushauri wako, sijui hata nifanyeje, huu ni mwaka wa 5 sasa nimekuwa najaribu kuingia kwenye mahusiano tofauti tofauti lakini naambulia kuachwa na kuumizwa. Mara ya mwisho nilikutana na mkaka mmoja ambaye tulianza nae mahusiano kwa haraka na motomoto sana lakini mwisho wake nikaja kuona anaanza kupunguza mapenzi taratibu, kaanza kupunguza mawasiliano na […]

509; Penda Tatizo Unalotatua.

Nipo natazama nyimbo YouTube nimekutana na wimbo uliwekwa mwaka 2009. Huo wimbo kwa mimi kuutazama leo pamoja na wengine wengi huyo mwimbaji atalipwa na YouTube (Google) mamilioni ya pesa. Nilichojiuliza ni kwamba huyu mwimbaji wakati anatunga wimbo huenda hakuwahi kuwaza kama mwaka huu 2019 huo wimbo wake bado ungeendelea kuingizia pesa. Nataka niseme na wewe […]

508; Atawainua Kunguru Wakulishe.

1 Wafalme 17:4,6 [4] Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 6. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito. Nimewatafakari wale Kunguru waliomlisha Elia nyama na mkate tena kipindi ambacho nchi ilikuwa imekosa mvua karibu miaka mitatu (maana yake kulikuwa na njaa) […]

507; Yanapotokea Usiyoyatarajia.

Ni kweli mtu unaweza kuwa na fikra hasi juu ya Maisha yako lakini hakuna mtu hata mmoja anaetaka zile fikra hasi zitokee. Kinachomfanya mtu ajikute anawaza sana ni kwasababu ya hofu. Kila mtu huogopa pale anapowaza mambo mabaya yatatokea siku moja, kila mmoja anaweza kusita kuchukua hatua pale anapohisi kuna jambo baya litatokea kwenye kile […]

506; Nilimwona Akiingia Gesti Jana Jioni

Ni mara ngapi umewahi kuambiwa kuhusu wengine, mfano; “Nilimwona Fulani akiingia Gesti Jana”, “Fulani ana Mwanamke Mpya” na mengine mengi. Ukweli ni kwamba huenda umeyasikia sana kutoka kwa watu au hata wewe ulishawahi kumwambia mtu. Sasa nikwambie kitu kimoja, hayo ni maoni tu ya watu ambayo hayana ukweli halisia. Ngoja nikupe kisa hiki, Miaka michache […]

505; Mama Usimtukane Mwanao.

Nilikuwa napita katika mitaa ya uswahilini hapa Tandika, sasa nikakutana na mama mmoja anamwogesha mwanae wa kiume. Sasa yule mtoto akawa anasumbua sumbua, yule mama akamporomoshea matusi mazito ya nguoni. Yaani alimuita viungo vyake yeye mwenyewe vya siri, nilisikitika sana, nikawaza huyu mtoto akija kupata akili sawasawa akaja kujua maana ya kile anachotukanwa na mama […]

504; Nyama Kilo 1 ni Tsh elfu moja.

Embu jiulize leo bei ya nyama kilo moja ni Tsh elfu tano hadi elfu saba kulingana na maeneo, sasa ukipita mahali ukakuta kuna nyama ya ng’ombe safi kabisa imenona wanauza kilo moja shilingi elfu moja utavutiwa kwenda kununua? Jibu rahisi sana na ambalo kila mmoja atafanya ni HAPANA. Na itakuwa hapana kwasababu haiwezekani nyama iuzwe […]