HATUA YA 379: Ni Kipi cha Muhimu Kwenye Maisha Yako?

Kipaumbele kikubwa kwenye Maisha yako ni kipi? Ndugu yangu kama huna kipaumbele kikuu cha Maisha ambacho ndio kinakuwa sababu ya wewe kuamka mapema, kufanya kazi kwa bidii utakuwa unapoteza muda. Lazima Rafiki uwe una kitu cha muhimu la sivyo Maisha yako yatakuwa ni dharura tu. Usiishi Maisha ya kufanyia kazi vitu vya dharura vinavyotokea kwenye […]

HATUA YA 378: Kama Ukiamka Asubuhi Unafanya Kitu Hiki, Upo Kwenye Hatari Kubwa Sana.

Muda wa asubuhi ndio wakati ambapo akili yako inakuwa na uwezo Mkubwa sana wa kufikiri na kufanya maamuzi magumu. Kama ukiweza kuutumia muda huu vizuri kufanya yale ya muhimu kwenye Maisha yako utakuwa na maendeleo makubwa sana. Watu wengi wanapoamka asubuhi kitu cha kwanza kufanya ni kushika simu zao kuangalia ni nani amewapigia au kuwatumia […]

HATUA YA 377: Fanya Kinyume Nao

Angalia kile watu wengi wanafanya kisha wewe fanya kinyume na wao na utaweza kuwa na mafanikio makubwa. Kama watu wengi hawaamki mapema basi wewe amka mapema kuliko mtu mwingine yeyote. Kama watu wanakuwa bize na simu zao kwenye magari wewe kuwa bize ukisoma kitabu au Makala kama hizi ambazo zitakufanya uwe bora Zaidi. Kama watu […]

HATUA YA 376: MAONI YA MTU MMOJA.

Umewahi kuwa na wazo lako zuri sana ambalo linakuhamasisha mno ukakutana na mtu mmoja ukamuelezea na kwa sentensi yake moja aliyokujibu ikakufanya ukaliharibu kabisa wazo lako? Hii imewahi kunitokea mimi sio mara moja ila baada ya mud asana nikajifunza kwamba kila mtu anaona kwa namna yake ya tofauti. Nikajifunza kwamba kabla hujafanyia kazi maoni ya […]

HATUA YA 375: Na Hiki Pia Umeamua Wewe.

Unajua kwamba umeamua mwenyewe kufungua Makala hii na kuisoma? Hivyo basi Maisha ya kila siku ni mkusanyiko wa maamuzi ambayo unayafanya kila dakika na kila saa. Kila inapopita dakika kuna jambo umeliwaza na ukafanya maamuzi. Unaamua kukaa kwenye mitandao ya kijamii masaa kadhaa ukipitia mambo ya ajabu ajabu. Ulianza kwa kukumbuka vitu vya jana ukasema […]

HATUA YA 374: Weka Bidii Na Ubora Hata Kama Huoni Manufaa Sasa.

Mwaka 2004 nikiwa shule ya msingi Mdawi tulichelewa kuingia darasani mimi na wanafunzi wenzangu na tukachapwa sana viboko. Sababu ambayo ilitufanya tuchelewe kuingia darasani ilikua ni matunda ya mizambarau iliyokuwa nyuma ya shule bondeni. Mizambarau hii ilikuwa imezaa sana na kulikuwa na miti ya mizambarau Zaidi elfu moja kwenye bonde lile la shule yetu ya […]

HATUA YA 373: Mazao Yakiliwa Na Wadudu Shambani Sio Mwisho Wa Kilimo.

Habari Rafiki yangu, zimepita siku chache kidogo sijakuandikia Makala katika Mtandao wetu. Najua umekuwa unatamani sana kunisoma lakini haikuwa katika uwezo wangu kukuandikia kwa wakati huo. Nimerudi tena, ninaendelea kuandika, ninaendelea kuzungumza na wewe. Sijaacha kuzungumza na watu nilikuwa najaribu kitu kingine cha tofauti ili nione matokeo yake. Halafu Rafiki yangu najua unatumia mitandao ya […]

HATUA YA 372: Kama Ukiona..

Kumekuwa na watu wengi ambao wanaweza kuona makossa na matatizo juu ya vitu lakini ni wachache wanaweza kuchukua hatua na kuleta suluhisho. Badala yake wanabaki wakilalamika kwa kusema ingekuwa hivi ingekuwa vile… kama wewe umeweza kuona chochote hakipo sawa basi ujue hiyo ni fursa kwako kuleta mabadiliko mahali pale. Kama umeona kuna watu wanafanya kitu […]

HATUA YA 371: Fanyia Kazi Kilichopo Mbele Yako.

Hakuna kitu kibaya sana ambacho kinawafanya watu washindwe kwenda mbele kama historia mbaya ya Maisha yao. Mfano wewe kwenu tangu umezaliwa umekuwa unaimbiwa wimbo wa sisi ni maskini, kwetu hawajasomaga hata mmoja, kwetu hakuna mtu mwenye akili. Maisha yako yote yanakuwa yakiifuata ile historia ambayo umekuwa unaambiwa. Inawezekana umeshindwa kufanya vizuri kwenye vitu vingi maishani […]

HATUA YA 370:  Mtu wa Ndani na Mtu wa Nje.

Mtoto mdogo ndio binadamu pekee ambaye kile anachokifanya unaweza kuamini anakimaanisha kabisa. Hii ni kwasababu mtoto anakuwa hajajua chochote juu ya ukweli wala uongo, hajui kudanganya wala kuficha kitu. Mtoto mdogo ana Maisha yasiyo na hila ndani yake, anaishi kwa uhuru mkubwa kuliko binadamu wengine ambao tayari tumeshaingiza chachu ndani yetu. Kiwango hiki ndio kiwango […]