HATUA YA 359: Umeifahamu Malighafi Sahihi?.

Tumekuwa na watu ambao wanapenda vitu ambavyo vipo tayari tayari. Kila wanachokitaka wanataka kiwe tayari kimeshakamilika na wao waanze kutumia tu. Ukweli ni kwamba tangu mwanzo tunaona asili ya vitu vingi ambavyo vinaonekana ni vichache ambavyo vimekuwa vimekamilika. Kila ambacho umekuwa unakitamani au unataka kukimiliki ni lazima ukubali kufuata mchakata wa kutengeneza. Unataka mke/mume mwenye […]

HATUA YA 358: Hiki Ndio Kitu Pekee Kinachopatikana Bila Bidii

Majani yanayojiotea yenyewe kwenye mashamba ambayo hayajapandwa kitu au hata yale yaliyopandwa mar azote huwa ni kwa ajili ya viumbe wengine ambao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao binafsi. Hii ndio asili na ndio maana popote pale penye udongo mzuri ukipaacha bila ya kupanda chochote patatokea majani ya aina mbalimbali. Wewe kama binadamu ni aina […]

HATUA YA 357: Watakukata Mbawa Zako.

Kuku na tai hawawezi kuishi pamoja na ili waweze kuishi pamoja njia ambayo ni rahisi sana ni tai kupunguziwa mabawa yake yanayomwezesha kuruka. Hii ni kwasababu kuku hata akijifunza vipi kuruka hataweza kwasababu mabawa yake hayamwezeshi yeye kuruka. Vilevile kuku hajaumbwa aweze kuruka hewani. Kuna aina ya watu ambao ukiishi nao lazima ukubali kuwa kama […]

HATUA YA 356: Kujua Mtoto Atazaliwa Haitoshi.

Mama anapobeba ujauzito kwa kawaida inajulikana kwamba ni baada ya miezi 9 ndipo mtoto huzaliwa. Kadiri muda unavyokwenda kuisogelea ule mwezi wa 9 ndipo shauku huwa kubwa juu ya kupokea mtoto. Kitakachowafanya wawe na nguvu kubwa Zaidi ya kufurahia mtoto ajaye ni pale daktarin anaposema mtoto atazaliwa tarehe 25 au 26. Vile vile kwenye Ndoto […]

HATUA YA 355: Epuka Ugonjwa wa Kutaka Kuwa Sahihi/Kutaka Kueleweka na kila mtu.

Umeshawahi kujikuta unafanya kitu kimoja na hukimalizi kwasababu kila ukikitazama unakiona kama hakijakamilika bado? Umeshakutana na hali ya kutaka kila kitu kiwe kiko sawa ndio uanze kuchukua Hatua? Umepata wazo la kuanzisha biashara unaanza kuogopa “nikianza kabla sijaitengeneza vizuri sana ninaweza nikashindwa.” Au huu wimbo naona bado haujanivutia sana ngoja nirudi studio tena, au hichi […]

HATUA YA 354: Usijipe Tafsiri ya Mabaya.

Unaweza kupitia hali mbaya muda mrefu kwenye Maisha yako hadi ukaanza kujiona wewe ni yule mtu ambaye anapitia hali mbaya. Unaweza kuwa umeshindwa kudumu kwenye mahusiano na watu mbalimbali kiasi kwamba ukaanza kujiona wewe ndio uko hivyo yaani wewe haukaagi kwenye mahusiano muda mrefu. Inawezekana pia hadi sasa umeshafanya biashara nyingi na zote zimefeli yaani […]

HATUA YA 353: Uko Vile Ambavyo Unajiona.

Haijalishi sana watu wanasema au wanajua wewe ni nani kuliko vile ambavyo wewe binafsi ndani yako unavyoamini. Wapo wengi wanaweza kukusifia au kukuona hufai kama wewe binafsi utakuwa hujioni unafaa yote hayo hayatasaidia. Unapaswa kutengeneza yule mtu ambaye unataka kuwa, andika vile ambavyo unajiona katika mtazamo chanya. Vile ambavyo ungejisikia vizuri Zaidi ukiwa hivyo. Imani […]

HATUA YA 352: Unachokikwepa Sasa Hivi…

Kiumbe hai chochote kina Hatua mbalimbali za ukuaji ambazo kinapitia hadi kufikia sehemu ambayo inakuwa ni ya ukomavu. Ili kiumbe hiki kije kuwa na mwisho mzuri lazima Hatua hizi zifuatwe kwa utaratibu. Huwezi kusema umepanda mahindi leo na ukayawekea mbolea na dawa le oleo ili yakue kwa haraka. Ukikimbilia kuyawekea mbolea mapema au ukayanyeshea maji […]

HATUA YA 351: Ukianza Kuona Una Sababu Nyingi…

Mwanadamu siku zote hapendi aonekane anahusika na makossa yake mwenyewe. Na inapotokea amekosea au ameshindwa jambo Fulani anatafuta mtu wa kumbebesha yale makossa yake. Tangu mwanzo wa kuumbwa kwa dunia tunaona Adamu na Hawa walipopatikana na kosa la kula tunda la mti walioagizwa wasile kila mmoja alianza kutoa sababu za kwanini alifanya vile. Adamu ambaye […]

HATUA YA 350: Kama una Imani ya Aina Hii Utapata Tabu Sana.

Imani huja kwa kusikia, tunasikia vitu vingi sana tunavyovihitaji na tusivyovihitaji kabisa kwenye maisha yetu. Kile unachokipa nafasi ya kukisikia zaidi kinajenga imani ndani yako. Kama unafuatilia kufanikiwa, unasikiliza na kusoma mafundisho ya mafanikio unajenga imani katika Mafanikio. Kama utawekeza muda wako katika kufuatilia bahati nasibu, kubeti, kufanikiwa kwa ghafla na imani yako itajengwa huko. […]