KONA YA BIASHARA: Unaona Nini?

Chochote unachokifanya sasa hivi kwenye biashara yako lazima kiwe kinafuata ile picha kubwa uliyokuwa unaijenga wakati unaanza. Usikubali kutoka nje ya picha ile hata kama mambo yanakwenda magumu sana. Endelea kuitazama ile picha ikupe hamasa Zaidi. Unapopitia magumu huwa unaona nini? Watu wengi huona kushindwa, kufilisika, kuanguka kibiashara, lakini leo nataka ubadili namna unavyoona wakati […]

KONA YA BIASHARA: Sababu za Kudumu na Sababu za Msimu.

Nimekuwa nakutana na watu wengi wanatamani sana kuingia kwenye biashara ukija kuwauliza ni kitu gani hasa kinawasukumu waingie watakwambia kuna matatizo Fulani wanataka wayatatue. Sasa watu wa aina hii wanakuwaga ni majanga sana kwasababu ataanza baada ya muda Fulani watu wamemzoea hivi yeye anakuwa amemaliza shida zake anaacha biashara. Vilevile anaweza kukutana na changamoto kidogo […]

KONA YA BIASHARA: Mabadiliko Yanakuja Utabaki Salama?

Kwenye chochote kile ambacho unakitegemea katika kukuletea pesa iwe ni biashara au ajira  ni vyema kujiuliza swali hili kwamba, kutokana na mabadiliko yanayokuja kila wakati hasa ya kiteknolojia je nitabaki salama kwa muda gani? Kama ni biashara basi angalia jinsi unavyoiendesha biashara yako sasa hivi na namna ambavyo mambo yanabadilika je unabadilika au unaendelea kutumia […]

​KONA YA BIASHARA: Usiyumbishwe na Mawazo Mapya.

Ukiamua kuwaza juu ya mawazo ya biashara na ukaweka ufahamu wako vizuri kila sehemu utakayokwenda utakuwa unaona fursa na mawazo mbalimbali ya biashara. Kitu kimoja kinaweza kukupoteza ni pale utakapotaka kutamani kufanya kila kitu. Kila wazo linakojua kichwani kwako unaona ni zuri na litakupa pesa unataka ulifanye. Mwisho wa siku unajikuta hata lile ambalo ulianza […]

KONA YA BIASHARA: Jipe Muda wa Kusubiri matokeo

Utaishia Kuwa mtu wa kuvunjika moyo siku zote kama utakuwa unatarajia mambo yaende kama vile ulivyopanga na unavyotaka. Siku zote tunapanga na tunatarajia lakini mambo yanaweza kuja tofauti. Mambo kuja tofauti haitakiwi iwe sababu ya wewe kukata tamaa na kuikimbia biashara. Kumbuka kwmaba ndio unapanda mbegu. Umeanza biashara yako ukajiwekea malengo makubwa na matarajio makubwa […]

KONA YA BIASHARA: Kwanini Unafanya Hiyo Biashara?

Mojawapo ya vitu vinavyofanya biashara nyingi zikwame au zifike mahali zikose mwelekeo ni wengi kutokujua kwanini wapo kwenye biashara wanazofanya. Wakati mwingine unaweza kujua kwanini lakini hicho kinachokufanya uwepo kwenye biashara kikawa ni kikwazo kwa biashara yako kukua. Kama utaanza biashara kwasababu umesikia kwa watu kwamba inalipa jiandae kuishia njiani. Kama utaanza biashara kwasababu kuna […]

KONA YA BIASHARA: Hii Ndio Njia Pekee Itakayokusaidia kupata Wateja Wa Kudumu.

Sifa ya binadamu ambayo tumejijengea na ni kubwa sana ni pale kujenga mazoea Fulani na mazoea yale yanakuja kuwa tabia zetu. Na siku zote mtu anapokizoea kitu anaweza kukichukulia cha kawaida sana na asikipe tena thamani yake. Unapotaka kuwa na bidhaa ambayo watu watahitaji sana kwenye maisha yao na wasiipate mahali kwingine unakuwa umejijengea namna […]

KONA YA BIASHARA: Mbuyu Ulianza kama Mchicha.

Nionyeshe mti mmoja imara ambao umekua kwa siku chache. Ukweli ni hakuna miti mingi ambayo hukua haraka haidumu wala mashina yake sio imara kama miti inayochukua muda mwingi kukua. Usitamani matokeo makubwa ya haraka ambayo hujayafanyia kazi utakuja kushindishwa kuyabeba au kuendeleza. Kama ambavyo tunasema mbuyu ulianza kama mchicha basi hakuna haja ya kukimbizana na […]

KONA YA BIASHARA: Biashara za Kufanya Kama Huna Mtaji Kabisa.

Unapokuja na sababu ya kwamba kinachokuzuia ni kukosa mtaji unakuwa umeizuia akili yako haki yake ya msingi kabisa ya kufikiri. Kwenye mazingira uliyopo kama una watu kumi tu wanaokujua na wewe unawajua hao wangetosha kuwa wateja wako wa kwanza kwenye biashara yako mpya. Moja; Kama watu hao kumi kuna kitu cha aina moja wanatumia labda […]

KONA YA BIASHARA: Epuka Tabia Hii

Jambo Moja unalopaswa kukumbuka kila wakati unapokuwa kwenye biashara yako ni hili EPUKA MAZOEA. Mazoea ni sumu mbaya sana ambayo inaweza kukusababisha ukaanza kumtafuta aliekuloga kumbe chanzo ni mazoea. Unapoanza biashara unakuwa na hamasa kubwa unawahudumia watu vizuri sana sasa shida inakuja pale unapokuwa tayari umeshasimama. Biashara inaenda vizuri umepata wateja wa kutosha na biashara […]