SURA YA 431; Tai Alievunjwa Mbawa.

Siku Moja Mzee aliekuwa anafuga kuku kwenye Kijiji fulani, alikuwa anapita porini akaokota yai kubwa ambalo hakuelewa ni la Ndege gani. Aliamua kulichukua yai lile na kuliweka katika mayai yaliyoanza kuatamiwa siku za Karibuni. Baada ya siku kadhaa kupita yule kuku akawa anatotoa mayai yake na kama muujiza hivi na lile yai kubwa likatotolewa. Kumbe […]

SURA YA 430; Huwezi Kumkwepa Mtu Huyu.

Unaweza kumdanganya kila mtu kadiri ya uwezo wako lakini yupo mtu mmoja ambaye siku zote atakuwa anakutazama na kusikitika kwa kile unachokifanya na mtu huyu ni wewe. Unaweza kujaribu kukwepa watu ambao umewafanyia ubaya, ukawakimbia wanaokudai, ukawakimbia wanaokusema vibaya lakini wewe binafsi huwezi kujikwepa. Hivyo basi mtu ambaye unapaswa kuhakikisha anakuwa mtu mwema, anaewapenda wengine, […]

SURA YA 429; Unaongozwa na Akili Yako, Ikidhoofu Itakuongoza Wapi?

Matendo yetu yote yanaongozwa na akili kama  akili zetu zitakuwa hazina afya basi tutakuwa tunapata matokeo mabovu kila wakati. Unaweza kuendelea kulalamika kuwa hupati matokeo unayoyataka lakini nakusihi uanze kutazama akili yako huwa unaijaza vitu vya aina gani. Kile kilichojaa sana kwenye akili yako ndio kinakuwa sababu ya matokeo unayopata. Mwaka huu punguza kabisa vitu […]

SURA YA 428; Ukitegemea Hiki Pekee Utachoka Haraka.

Mwanadamu pekee aliekuwa na akili sana kuliko wanadamu wengine ni Adamu na yeye alipewa uwezo huo kwasababu alikuwa peke yake. Hivyo kwa akili na uwezo aliokuwa nao ukamuwezesha kuyaendesha Maisha yake kwa urahisi. Kwasasa kila unachotaka kukifanya kwa kiasi kikubwa kinategemea wengine, inawezekana ni vifaa, au hata watu wengine utawahitaji ili uweze kuwa na ufanisi […]

SURA YA 427; Njia Rahisi ya Kuwavuta Watu Sahihi Kwako.

Tupo kwenye dunia ambayo ni ngumu sana kumjua mtu kwasababu wengi wamevaa mavazi yanayofunika uhalisia wao. Wamevaa tabia za kuigiza ambazo sio za kweli na wala hawana kabisa. Wamevaa Maisha ambayo ni uongo na ndani yake wanateseka huku wakifurahia kuona watu wanawasifia. Sasa ili uweze kuwavuta watu sahihi na kuwaacha hawa waliojivalisha mavazi ya uongo […]

SURA YA 426; Hii Ndio Sababu Ya Wewe Kuanza Vizuri na Kumaliza Vibaya.

Hongera sana kwa kuona mwaka mpya, nafurahi pia kuona umesoma Makala hii kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2019. Nimekuwa nahudhuria mikesha na matamasha ya kuingia mwaka mpya na siku zote nimekuwa najifunza kitu ambacho kimekuwa kinajirudia sana. Hakuna mwaka ambao umewahi kutabiriwa mabaya, na hata kama watasema utakuwa mwaka wenye magumu lazima watayataja mazuri […]

TUSEMEZANE 425; MAMBO 37 YA NILIYOJIFUNZA MWAKA 2018.

Habari Rafiki nimekuwa na utaratibu wa kukuandikia mambo niliyojifunza kila mwaka na mwaka huu hii ndio mojawapo ya mambo ya muhimu kabisa niliyojifunza na ningependa nikushirikishe na wewe. 1 Hakuna kisichowezekana usiipe akili yako kikomo au kusema mimi siwezi hiki. 2 Usipofanya maamuzi magumu hutatoka hapo ulipo hata siku moja. 3 Penda kujaribu vitu ambavyo […]

TUSEMEZANE 424; Ukimpata Usikubali Aondoke.

Katika Maisha tunakutana na watu wa aina mbalimbali wanaweza kuwa wabaya kwetu na wengine huwa baraka kubwa sana kwenye Maisha yetu. Unaweza kukutana na mtu wa pekee sana kwenye Maisha yako na usiweze kujua kwasababu shetani amefunga ufahamu wako usione huyu mtu ni wa namna gani. Ni vyema ukawa na uwezo wa kufahamu wale watu […]

NGUVU MPYA 423; Usikae Hapo Muda Mrefu Sana.

Unaweza kufanya mambo makubwa kwenye Maisha yako na ukashindwa kusogea mbele tena kwasababu moja ya kulewa na yale matokeo. Jambo ambalo tayari umeshalifanya na ukashinda halitakiwi liwe ndio jambo unaloliongelea sana kwamba umelifanya. Waachie wengine walizungumzie wewe nenda katafute jambo jingine kubwa Zaidi la kufanya. Sijasema usifurahie matokeo uliyopata bali nasema usifurahie sana hadi ukasahau […]

NGUVU MPYA 422; Eneza Habari Njema.

Watu wamekuwa ni mashujaa sana wa kueneza habari mbaya kuhusu wengine, imekuwa ni desturi yetu pia kutoa vipaumbele Zaidi kwenye habari mbaya kuliko njema. Wafuatiliaji wa habari na watoaji wa habari wote wamekuwa wakipendelea Zaidi habari mbaya. Kwenye Maisha yako kama unataka kufanya jambo lenye kuacha alama basi chagua kusema kile ambacho kinawasaidia wengine. Habari […]