JINSI YA KUANZIA CHINI KABISA NA BIASHARA YAKO

Habari za leo Ndugu. Unaendeleaje na katika kutafuta Maisha ya mafanikio? Leo nimekuletea mada nyingine ya muhimu sana baada ya mada ya mada ya mtaji. Haya mambo mazuri tunayozungumza hapa njia nzuri ya kupata matokeo ni kufanyia kazi haya unayojifunza bila kukata tamaa. Haijalishi utakutana na changamoto kiasi gani unatakiwa uendelee kupambana uzivuke ili ufikie […]

Tabia Ya Uvumilivu Ni Muhimu Ili Ufanikiwe

Habari ya leo ndugu Msomaji. Ni matumaini yangu unaendelea vyema katika mapambano yako ya maisha. Tunaendelea na mfululizo wa Makala za tabia kwasababu mafanikio yeyote yanaletwa na tabia mbalimbali zinazojengwa kwa kurudiarudia kila siku. Kuna vitu ambavyo hutakaa uvisahau maishani mwako hata ukiwa umelala kitandani unaumwa. Mfano ni silabu, a, e, i, o, u hizi […]

MAMBO 5 YA MUHIMU ILI UWEZE KUFIKIA NDOTO ZAKO.

Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na kupambana katika kutimiza ndoto zako. Leo ninakwenda kukupa njia mambo ya muhimu sana ili wewe uweze kuzifikia ndoto zako na maono yako.   Jua kusudi lako Tunajua kabisa ili uweze kuishi maisha yenye furaha na utimilifu kwanza ni kulijua kusudi lako. […]

Jikubali Mwenyewe Kwanza.

Kabla wengine hawajaona kilichopo ndani yako ni vizuri zaidi ukawa wa kwanza kukiona na kukijua vizuri. Kabla wengine hawajaanza kukusifia jisifie Mwenyewe  na hapa simaanishi mbele za watu hapa ni wakati ukiwa Mwenyewe chumbani. Kabla wengine hawajakwambia unaweza anza kujiona unaweza, jiambie naweza jione ukiweza jione ukipiga hatua mbele Zaidi. Wewe ni mtu wa pekee […]

Jinsi ya kupata wazo la biashara:

Habari za leo ni matumaini yangu kua unaendelea vyema kabisa. Leo tunakwenda kutazama njia tano za kupata wazo la biashara popote pale ulipo. Karibu ujifunze nami. Zipo njia tano ambazo unaweza kuzitumia kubuni wazo bora la biashara katika jamii uliyopo nayo ni: •       1. Kwa kuangalia baadae(future): Kwa kuangalia jamii unayoishi unaweza kugundua baadae mabadiliko yatakuaje […]

JIPONGEZE.

Unapotimiza malengo yako haijalishi ni madogo kiasi gani unatakiwa ujipongeze. Kwanini ujipongeze?  Hii inakuongezea hamasa zaidi ya kufanya mambo mengine yanayoendelea. Haijalishi ni Hatua gani umefikia jijengee tabia hii ya kujipongeza mwenyewe hakuna mtu mwingine atakuja akupe pongezi sana sana utaambiwa hongera. Jipatie zawadi ndogo ndogo zile unazozipenda. Haina maana kwamba ukajipe zawadi kubwa ya […]

Kusita sita ni Adui wa mafanikio yako. 

Kama Unaogopa hatari, hasara, kupoteza, hautakaa uweze kutoka hapo ulipo. Hautawezw kusogea mbele. Maisha ni kujitoa na kufanya bila kuogopa chochote bila kuogopa changamoto. Kuna vitu huwezi kuvizuia kutokea katika maisha yako na kuna ambavyo unaweza kuvizuia. Usivyoweza kuvizuia Achana navyo wala usivipe nafasi ya kukuzuia wewe kufanya jambo. Jinsi unavyozidi kusita kufanya maamuzi ndivyo […]

#SiriZaKuaHaiLeo:1. Ni nafasi ya kubadilisha.

Ni nafasi nyingine ya kutubia makosa yako. Ni nafasi nyingine ya kufanya upya kwa umakini pale ulipokosea jana. Ni nafasi nyingine ya kufanya uchaguzi upya. Yako mambo mengi tumechagua jana kwa makosa mengine yana uwezekano wa kuchagua upya leo ndio wakati wake. Ni nafasi nyingine ya kipatana na uliowakosea. Inawezekana jana umekwazana na watu leo […]

Walioshindwa.

Walioshindwa jambo na wakaliacha kabisa bila kurudia au kujua kwamba wao wanahusika vipi katika kushindwa kule, wana maelezo ya kutosha kukushawishi na wewe kwa nini utashindwa. Jihadhari sanaa na watu hawa maana wana uwezo mkubwa wa kuondoa hamasa yako juu ya jambo unalotaka kuliendea. Waelewe hivi: Walishindwa kwasababu ya uelewa wao mdogo juu ya jambo […]

UNAHITAJI WATU.

Mwandishi mmoja wa vitabu anaejulikana kwa jina la Zig Ziglar Alisema “To get what you want you must help enough people to get what they want”  yaani kupata chochote unachotaka unahitaji kuwasaidia watu kupata vile wanavyotaka. Akiwa na maana kwamba kile unachokifanya kiwe kinagusa maisha ya wengine. Kama biashara unayoifanya haigusi maisha ya watu wengine […]