Pale unapohisi.

Pale unapojihisi kukata tamaa ndio sehemu hasa ya kuongeza bidii maana ni matokeo yanavyokwenda kuonekana. Pale unapojihisi kuchoka ndio wakati wa kuinuka tena kwani vita ndio imeanza mapambano ndio yamechanganya uchague kurudi nyuma upotee kabisa au upambane hadi mwisho. Pale marafiki zako wanapokucheka na kukwambia umepotea ndio wakati hasa wa kuonyesha unajiamini na unakiamini vyema […]

Tabia za watu wenye Mafanikio.

Tabia ni vile  vitendo ambavyo tunavifanya mara kwa mara bila kuacha. Tabia ni vitu ambavyo vimejengeka ndani yetu, kama unavyoweza kuamka na kuswaki kila siku asubuhi bila kuchoka wala kukata tamaa. Kuswaki na kunawa uso asubuhi nayo ni Tabia. Sio rahisi uache na wala ujisikie kuchoka. Hii ni kwasababu umerudiarudia hadi ikajijenga kwenye akili yako […]

Nguvu ya Ulimi.

Wanasema Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini kinaweza kufanya mambo makubwa. Ulimi unaweza kuvunja ndoa yako. Ulimi unaweza kukukosanisha na ndugu jamaa na marafiki. Ulimi unaweza kukupeleka jela. Ulimi unaweza kujenga mahusiano mazuri na watu. Ulimi unaweza kukupatia kazi nzuri sana. Ulimi unaweza kubadilisha maisha yako Leo. Unatumiaje kiungo hiki ili kupata manufaa zaidi kwenye […]