Category Archives: VITABU

KITABU: NUKUU ZA MAISHA.

Nukuu za Maisha (Malengo, Mafanikio, Mahusiano n.k) ni Kitabu kinachokupa muongozo wa maneno ya kutafakari kila siku asubuhi ili uweze kuwa na siku bora na yenye mafanikio.

Kitabu hiki kina nukuu 400+ ambazo zinakupa uwezo wa kufikiri vizuri, kuishi kwa furaha na kuweza kusonga mbele katika kile unachokifanya.

Nukuu za Maisha ni mjumuisho wa nukuu za furaha, nukuu za mahusiano, nukuu za upendo, falsafa za maisha, nukuu za mafanikio, nukuu za biashara, nukuu za hamasa, nukuu za malengo, nukuu za kutia moyo, nukuu za kuongeza ujasiri, nukuu za kuongeza kujiamini na kadhalalika usiache kusoma kitabu hiki.

NUKUU ZA MAISHA ni mkusanyiko wa nukuu ninazoandika kwenye mtandao wa Instagram kila siku. Nimezikusanya zaidi ya 400 na utaweza kuzisoma kwenye kitabu kimoja.

SHUHUDA ZA NUKUU HIZI KWENYE MAISHA YA WATU

Hakika nimesoma maandiko yako mengi sana nimepata mafanikio makubwa sana kifikira sasa nimeweza kukaribia malengo niliyojiwekea Mungu akutie nguvu. Pia baada ya kumaliza kusoma kitabu cha USIISHIE NJIANI nimejifunza mambo mengi sana.

EvaStella Ricknelson

Tangu nimeanza kufuatilia NUKUU za Jacob kwenye mitandao ya kijamii nimeona mabadiliko makubwa, nimekuwa jasili, najiamini, napambana sana kwenye utafutaji wangu, na nimejifunza kuto kukata Tamaa.

– Stella Samwel

 Katika nakala zako na jumbe zako zimenifungua macho maana Nilikuwa sioni wapi ninapokwenda katika maisha yangu yapo Mambo mengine niliyaona hayawezekani lakini leo nayaona yanawezekana.

Elisha Dismas

Ni kweli nimepata vitu vingi toka kwenye nukuu zako za Maisha! Ukweli ni kwamba maisha halisi ni Maarifa, uko vizuri, zidi kutafuta maarifa utaishi ndoto zako pia ukimtanguliza Mungu mbele maana Zawadi na vitu vingine vyote vyatoka kwa MUNGU

Justin Kabembo

 “Tangu nimeanza kufuatilia NUKUU za Jacob kwenye mitandao nimeona mabadiliko makubwa kwenye Maisha yangu. Kwanza nimeamini maisha ni kuthubutu. Pili kila jambo linaanzakufanikiwa katika akili yako. Tatu, Matendo yako yanakuwezesha kutengeneza ile picha uloifikiria kuwa halisi. Nne, rafiki/mchumba/mke/mume ni chachu ya mafanikio au changamoto za mafanikio yako. Hivyo chagua maisha!!

Joshua S. Lebabu

Tangu nimeanza kufuatilia Makala zako nimekuwa nikipata maneno mazuri ya faraja ya kutokukata tamaa katika safari ya mafanikio

Prosper Cosmas

Tangu nimeanza kusoma nukuu na vitabu vya jacob Mushi. Nimepata mwanga mkubwa sana nimekuwa mtu mwenye upeo na maono makubwa kimafanikio, japo ni katikati lakini angalau nimekuwa mfano wa kuigwa. Isitoshe Jacob amenishauri mambo mengi ya kimaisha na kibiashara. Ni miongoni mwa waandishi bora hapa nchini. Hakika huwezi Jutia ukisoma nukuu na vitabu vyake.

Denis Tesha

Tangu mwaka 2016 nilipoanza kukufuatilia umenifanya niwe mtu mpya Na niweze kufanya mambo ambayo sikutegemea kuwa yanafanyika.

Baraka MWAMPULULE

“Kwakweli nukuu zako zinatoa mwanga mpya na kutia moyo kwa walioanguka wainuke na kuendelea.”

Mtaalam Md

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kukuleta maishani kwangu Kaka, hakika umekua sehemu ya mabadiliko katika nyanja tofauti tofauti maishani mwangu, Vitu vingi Sana nimejifunza na ninazidi kujifunza kutoka kwako, umenifundisha ujasiri wa kuthubutu, umenifundisha namna ya kuyatumia matatizo Kama fursa ya kuingiza kipato, namna ya kuishi na watu, ni  mambo mengi sana, Hadi mda huu naona utofauti mkubwa Sana katika maisha yangu tofauti na nilivyokuwa mwanzoni, ubarikiwe Sana na uzidi katika Hilo.

Peter Mahunja.

Nimejifunza Ni jinsi gani ninaweza kujisimamia binafsi.

Kareem

Tangu nimeanza kusoma kazi zako, Vitabu na kwa blog pamoja na nukuu nimejifunza vingi vya kunipa hamasa ya kusonga mbele na zimechangia kubadilisha maisha yangu kifikra kwa kiasi kikubwa.

Peter Mbizo

Binafsi mimi makala zako zimenifanya niwe mtu wa kujiamini na kufanya kila kitu bila kukata tamaa na kuwa mtu subira maana Hapo mwanzo nilikuwa mtu wa wasiwasi na muoga wa kujaribu kufanya kitu asante sana kwa makala zako za kutia moyo.

Nelson Frank Mushi.

Hata pasipo ya kuniuliza ni mabadiliko gani nimeweza kuyapata kupitia kufuatilia nukuu hizi ningelikuambia siku moja kuwa ama hakika wewe ni nabii ulikubalika kwenu. Nukuu zako zimenijenga sana katika swala la kutokujikatia tamaaa kulingana na hali za maisha niyoyaishi kila siku ni hii ni baada ya kusoma jarada lako moja kuhusu maisha ya Daud pamoja na wazazi wake hadi kuufikia ufalme.

Steven Samwel

Nashukuru mno Bro kwa kweli Mimi ni mdau wako namba moja, mafundisho yako yanafariji na kukufanya mtu ujitambue, Kama Kuna sehemu ulisinzia basi ghafla unaamka, mie ni single mom kwa hiyo Niko na changamoto nyingi ninazopitia katika kujikwamua, Kuna muda nakuwa na stress ghafla nikikusoma naona Kama wasema Mimi, basi napata funzo na kupiga hatua nyingine.

Rehema Lebby

 

Tangu nimeanza kusoma kusoma kitabu chako nimejitambua kwa kweli nimejifunza kuwa na mimi ninaweza kufanya jambo nikaweza kwa uelewa wangu nilionao, nimejifunza ni aina gani za marafiki natakiwa kuwa nao, ni mambo gani inabidi niyafanye ili niweze kutimiza maono yangu kwa kweli hiyo ni kwa ufupi lakini nimejifunza mengi na bado naendelea kuyatendea kazi.

Nuriath Nuru

Kiukweli bila kuficha toka nianze kufuatilia nukuu zako ndugu jacob mushi kuna mabadiliko makubwa kwangu. Kwanza kwasasa, najiamini, Sina hofu, Nathubutu, Siahirishi mipango, Nimekuwa na nidhamu Asante sana kwa nukuu zako.

Wille Balisho

Nadhani kila mtu hapa Duniani anahitaji mtu wakumtia moyo, inawezekana maneno ya mtu yakatosha nikiwa nasoma najitia moyo kwa maneno yako nakusonga mbele bila kuishia njiani.

Palmaraham Nkya

NAMNA YA KUPATA KITABU HIKI:

Bei ni Tsh 10,000/= hardcopy/softcopy,

Namba za Malipo.

0654 726 668 Tigopesa. Jacob Moshi,

KITABU: Mafanikio Kwenye Biashara.

Kitabu hiki kimebeba uhalisia wa Maisha ambayo nimeishi na kujifunza kutoka kwa wengine. Pamoja na kitabu hiki kubeba mambo mengi mazuri sana, bado inakupasa wewe uwe mchukuaji wa Hatua kwa kila unalojifunza ndani ya kitabu hiki. Usiishie kusoma na kuburudika kama msomaji wa hadithi bali uweze kuchukua Hatua hata kama ni ndogo lakini inayoleta mabadiliko kwenye Maisha yako.

Karibu sana Rafiki Yangu ujipatie maarifa haya na Maisha yako yabadilike.

Kitabu hiki ni kwa ajili yako wewe Rafiki yangu ambaye hadi sasa bado unasua sua na kutoa sababu kibao ambazo unataka zihalalishe kwanini hujaanza biashara hadi sasa. Pia ni kwa ajili ya wewe ambaye tayari ulishafanya biashara ukafeli kwa namna moja au nyingine. Kufeli huko kukawa sababu ya wewe kuacha kabisa na kuogopa kuanza tena.

Kitabu kimegusia maswali ambayo umekuwa unajiuliza mara kwa mara, kama, Jinsi ya Kufanikiwa Kibiashara, Namna ya Kuwekeza Katika Biashara, Biashara zenye Mafanikio ni zipi?, Siri za Wafanyabiashara wenye Mafanikio Makubwa Duniani, Funguo za Mafanikio Kibiashara, Kanuni za Kukuza Biashara, na mengine mengi.

Ni kwa ajili yako wewe ambaye uko kwenye biashara miaka na miaka lakini hukui. Biashara yako ni ile ile siku zote. Hakuna mabadiliko yeyote.

Kitabu Hiki Kimetoa Jibu la Maswali haya;

Kwanini Hujaanza Biashara hadi sasa?

Sababu ambazo watu wengi huzitumia kama kinga ya kwanini hawajaanza biashara na suluhisho za sababu hizo.

Kwanini Ulishindwa?

Sababu mbalimbali ambazo zimekuwa chanzo cha wewe kupata hasara au kushindwa kwenye biashara uliyoanza, na Hatua za kuchukua ili uweze kuwa mshindi.

Kwanini wewe Hukui Kama Wengine?

Chanzo cha wewe kudumaa kwenye biashara miaka na miaka bila ya mabadiliko yeyote. Hatua za kuchukua ili uweze kukua na kuongezeka.

Hizo ni baadhi ya mambo niliyogusia kwenye kitabu hiki. Unaweza kuona ni jinsi gani ambavyo unakwenda kupata suluhisho na kutoka katika ile sehemu ambayo wewe umekwama.

Kinapatikana kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya Tsh 10,000/= (elfu kumi). Ukishafanya malipo ya Kitabu tuma jina la kitabu pamoja na email yako na utatumiwa kwenye email yako mara moja.

Namba za Malipo.

0654726668 Tigopesa.

Karibu Sana Rafiki.

Jacob Mushi,

KITABU: Usiishie Njiani, Timiza Ndoto Yako.

Kitabu hiki ni maalumu kwako wewe ambaye unataka ndoto yako itimie.

Kitabu hiki ni kwa ajili yako wewe ambaye bado hujapata mwelekeo wa Maisha yako. Utapata mwongozo kwa ajili ya kujitambua.

Unapata Nini kwenye Kitabu?

Utafahamu Umuhimu wa Maono kwenye Maisha yako.

Utafahamu maswali 8 ambayo unapaswa kujiuliza na majibu yake ili uweze kusonga mbele.

a/. Kujitambua Wewe Ni Nani

b/. Kutambua Upo Duniani kwa Kusudi Lipi.

c/. Kujua Unapotakiwa kwenda.

d/. Kuwatambua Watu Wa Muhimu Kwenye Safari Yako.

e/. Kuzitambua Tabia Unazozitaji Kila Siku

f/. Utatambua Maarifa Gani Yanakufaa Zaidi.

Kitabu Hiki kinamfaa mtu ambaye ana ndoto kubwa na anatamani itimie. Kinamfaa mtu ambaye bado hajui kwanini yupo Duniani, na hana maono yeyote yale. Kitabu hiki kinakufaa sana wewe ambaye unatamani kutimiza ndoto yako.

Utaweza, Kutimiza Malengo Yako Kirahisi zaidi, Kuwajua Marafiki Sahihi, Kuishi Maisha ya Ushindi, Kurejesha Upya Nguvu Zako, Kufika katika Kilele cha Mafanikio,

Kinapatikana kwa kwa bei ya Tsh 5,000/= (elfu 5). Walioko mikoani tuwasiliane kabla hujalipia.

Namba za Malipo

0654726668 Tigopesa.

Karibu Sana Rafiki.

Jacob Mushi,

KITABU; Mbinu 101 za Mafanikio. – Jacob Mushi

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa makala ninazoandika kila siku za HATUA ZA MAFANIKIO. Nimechambua makala 101 ambazo ukizisoma zinaweza kukupa mbinu na maarifa ya kukuwezesha usonge mbele zaidi kwenye kile unachokifanya.

Kitabu hiki cha Mbinu za 101 za Mafanikio Kimejumuisha , Mbinu za Maisha na mafanikio, sms za mafanikio, siri ya mafanikio katika biashara, nguzo za mafanikio katika Maisha, siri ya mafanikio pdf, nini maana ya mafanikio, kitabu cha siri ya mafanikio, dira ya mafanikio, kanuni za kuwa Tajiri , njia kuu za mafanikio katika Maisha, historia ya matajiri duniani, tabia za matajiri, mbinu za biashara na utajiri, siri ya mafanikio, jinsi ya kupata utajiri kwa haraka, siri za matajiri duniani.

Utapata nafasi ya kuongezeka kwenye MAHUSIANO, BIASHARA NA ROHO YAKO PIA. Usiache kusoma kitabu hiki ili uweze kusonga mbele.

Kinapatikana kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya Tsh 10,000/= (elfu kumi). Ukishafanya malipo ya Kitabu tuma jina la kitabu pamoja na email yako na utatumiwa kwenye email yako mara moja.

Namba za Malipo. 0654 726 668 Tigopesa.

Karibu Sana Rafiki.

Jacob Mushi,

KITABU; Siri 7 za Kuwa Hai Leo

Kitabu hiki nimeandika kwa ajili yako. Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ndani ya kitabu hiki na nina imani kitakua ni sababu ya wewe kusogea katika eneo lile ulilokua na kwenda mbele Zaidi.

Utajifunza, Jinsi ya Kujua Kusudi Lako, Siri na Sababu za Kuwepo Hapa Duniani, Kugusa maisha ya wengine, Kufikia Ukuu, Kufika kilele cha Mafanikio, Kuishi maisha bora, Kutengeneza Na Mungu Wako, Kutambua kile Mungu ameweka ndani yako, Kufikia Ushindi Mkubwa.


Watu wengi wanaishi Maisha ambayo hayana mwelekeo, wanafanya kazi wasizozipenda, wanaishi Maisha wasiyoyataka kwa maana kuwa hayawapi furaha. Hii yote inaletwa na kutokujua sababu hasa ya wao kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kitakwenda kukufungua macho.

Utajifunza:

 • Kusudi la Wewe Kuwa Hai.

Ili uweze kuishi Maisha yenye mwelekeo mzuri na kujua ni kipi hasa unapaswa kufanya kila siku ni hadi utakapoweza kutambua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kimeeleza namna yaw ewe kugundua kusudi lako.

 • Kugusa Maisha ya Wengine.

Kila unachokifanya hapa duniani kinaongezeka sana endapo kitakuwa kinagusa Maisha ya wengine. Kiwango cha Maisha uliyogusa ndio kiwango cha mafanikio yako.

 • Kutengeneza Historia Mpya.

Ni alama gani unataka kuacha hapa duniani? Haijalishi umeshafanya makosa mangapi kuwepo kwako leo kunakupa nafasi ya kutengeneza historia mpya. Kitabu hiki kitakupa mwongozo huo.

 • Kuishi Maisha ya Ushindi.

Unatakiwa uishi Maisha ya ushindi kila siku kwenye kila unalolifanya. Utajifunza mbinu za kupata ushindi kwenye kila unachokigusa na mikono yako.

HAYA NI BAADHI YA MAONI MACHACHE NILIYOPATA KUTOKA KWA WATU AMBAO WAMESOMA KITABU HIKI.

“Kuwa Hai ni Zaidi ya kuwepo duniani, watu wengi sana wapo duniani lakini hawapo Hai, na wanaishi maisha ambayo si yao, Jacob Mushi kupitia Siri 7 za Kuwa Hai Leo ametengua kitendawili hicho, kwa kufichua mambo ya msingi ambayo ya kuishi maisha ya utoshelevu.”

Street Pastor,

Masanja Mkandamizaji

“Yaani ukianza kukisoma hutamani kuacha kwa jinsi kimebeba ‘facts’ Watu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa kumbe yamo kwenye “SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO.”  Ushauri wangu kwa Watanzania na wengine wanaoelewa kiswahili usikose nakala yako ya kitabu hiki kwenye library yako nyumbani. Thamani yake ni zaidi ya Tsh 10,000= utakayoitoa kukinunua. Hakika kitabadilisha maisha yako kuwa bora zaidi.”

Regula Tarimo

Mjasiriamali.

“Siri 7 za kuwa Hai Leo, ni kitabu kinachotoa muongozo wa kuishi maisha ya kulitimiza kusudi lako kwa mafanikio na furaha, Jacob Mushi amewasilisha kwa lugha inayoeleweka siri saba zitakazokufanya ujitambue na uanze kuwa hai. Kwa mtu yeyote mwenye kutaka kuishi maisha ya ushindi leo na kuacha historia nzuri napendekeza asome kitabu hichi.” 

Daudi Mwakalinga

Mkurugenzi/CEO wa kilimo.net.

“Kitabu cha Siri 7 Za Kuwa Hai Leo ni kitabu ambacho kila mtanzania hapaswi kukosa kukisoma. Nimekisoma na nimeona nguvu iliyoko ndani ya kitabu hiki pia nimeshuhudia watu wengi wakitoa sifa tele za kuweza kubadili maisha yao kupitia kitabu hiki. Napenda kusema kitabu hiki ni kama lulu kwa kila mtanzania kuweza kujifunza na kubadili fikra na maisha yake. “

Lazaro Samwel

Kocha wa Maisha, Mwandishi na Mjasiriamali.

Mtunzi na Mwandishi wa Kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA.

Email; lazarosamweli41@gmail.com

“Huwezi kusoma kitabu hiki kisha ukabaki kama ulivyo. Uwe unafanya kazi au hufanyi kazi uwe mfanyabiashara,  mjasiriamali au mwimbaji kama mimi, ukisoma Siri 7 za kuwa hai leo, ni lazima utaongezeka kwenda hatua nyingne.“

Atosha Kissava

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania

Kinapatikana kwa mfumo wa softcopy kwa bei ya Tsh 10,000/= (elfu kumi). Lipia kwenda namba Tigopesa 0654 726 668 jina lilatokea Jacob Moshi. Ukishafanya malipo ya Kitabu tuma jina la kitabu pamoja na email yako na utatumiwa kwenye email yako mara moja.

Karibu Sana Rafiki.

Jacob Mushi,

KITABU: Mwongozo wa KILIMO CHA TIKITI MAJI

Baadhi ya Yaliyomo kwenye Kitabu hiki:

 • Utajifunza shughuli zote za shambani kuanzia kuandaa shamba, upandaji, umwagiliaji, uwekaji mbolea, palizi, uvunaji n.k
 • Vigezo vya kuzingatia katika uchaguaji wa shamba zuri pamoja na mbegu nzuri
 • Utawafahamu Wadudu waharibufu na namna ya kuwadhibiti kikamilifu, pia Magonjwa yanayoathiri sana tikiti maji na namna ya kuyathibiti
 • Utajifunza uchavushaji (pollination) kwenye zao la tikiti maji na namna unavyoweza kuongeza uchavushaji na kuongeza mavuno hadi asilimia themanini (80%)
 • Masoko: Utaelewa mienendo ya bei, kipindi chenye bei nzuri, kipindi chenye bei mbaya na sababu zake. Hii itakusaidia kujua wakati sahihi wa kupanda zao la tikiti ili upate faida nzuri Zaidi.
 • Utajifunza namna unavyoweza kutumia simu yako kujua bei za tikiti kwenye masoko yote hapa Tanzania. Yaani bei za kila siku za kwenye masoko yote makubwa hapa Tanzania utaweza kuzijua kupitia simu yako.
 • Pia utajifunza namna ya kutafuta wanunuzi kupitia simu yako, yaani utajua namna ya kupata mawasiliano ya wanunuzi(namba zao za simu) kutoka masoko mbalimbali. Kwenye kitabu hichi utajifunza hayo yote.
 • Master plan: Hapa mwandishi amekuwekea mpangilio wa shughuli zote, tena hatua kwa hatua kuanzia kupanda hadi kuvuna. Utafahamu nini kianze na kipi kifuate. madawa yote, mbolea zote, na shhguli nyingine zote zipo
 • Uchambuzi wa gharama na Faida: Hapa utapata kufahamu rasilimali zote zinazohitajika na gharama zake, pia utajua faida utakayopata.

Namna ya Kupata nakala yako:

Kitabu hikikinapatikana katika mfumo wa hardcopy, kama upo mikoani utatumiwa kwa gari. Kama upo Dar utaletewa hadi ulipo.

Unafanya malipo ya 10,000  Tigo pesa 0654726668 (Jina Litaonyesha Jacob  Moshi)

Ukishafanya malipo unatuma Ujumbe wenye Jina na lako kwenda  au 0654726668.

Kama   na ungependa kutumiwa Kitabu kwa email, Whatsapp au Telegram basi utatuma ujumbe WhatsApp au Telegram kwenda namba 0654726668

Wahi Ujipatie nakala yako.

www.kilimo.net