Kwenye jambo lolote baya linalotokea kwenye maisha yako unaweza kuchagua kulalamika au Kuchukua Hatua.

Unaweza kuchagua wa kumlaumu, unaweza kujieleza sana jinsi ulivyo sahihi jinsi ambavyo wewe hujakosea au kuamua kukubali yaishe ili mambo mengine yaendelee.

Lawama hazibadili chochote.
Lawama haziondoi ukweli.
Lawama hazifanyi uonekane wewe hukukosea.
Hata ukiweza kulalamika vya kutosha hakuna kitakachobadilika.

Kama wewe unapenda kutafuta sababu, kulaumu, kulalamika, kujitetea ukweli maisha yako yatakua magumu sana na hakuna kitachobadilika.  Jifunze kuchukua hatua kwenye kila jambo linalotokea kwenye maisha yako  kama huwezi kubadili achana nalo usipoteze muda kulalamika kulaumu maana haibadili chochote.

Kaa mbali na watu wanaolalamika maana ni tabia ambayo inaambukiza haraka sana. Na tabia hii inakufanya urudi nyuma kimaendeleo.

Unapopata tatizo ukafikiri kwamba kuna mtu atatakiwa kukusaidia unajidanganya Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye yeye yupo kwa ajili ya kukutatulia matatizo yako. Kama umekwama na umetafuta suluhisho ikashindikana omba msaada na yule uliemwomba asipokusaidia pia ni sawa. Kwa sababu yeye hayuko ili kukutatulia matatizo yako acha kupoteza muda kumlaumu maana hata yeye ana matatizo yake,  unamjua anamwambiaga nani?

Acha kulalamikia serikali. Kuna watu ambao wanasema serikali ya sasa hali ni ngumu mambo hayaendi ni kweli lakini kuna ubachoweza kubadili?
Chochote kinachoendelea kwenye maisha yako wewe ndie mhusika mkuu acha kutafuta watu wa kuwatwika mizigo yako.
Tafuta Suluhisho.

Asante sana
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading