Katika Jambo lolote unalotaka kulifanya kwenye dunia hii. Lazima ukutane na watu wa aina tatu. Hata kama unaenda kuuza nyanya leo hawa watu Lazima uwakute.
1. Ambao hawajawahi kufanya hicho kitu kabisa.
Watu hawa wanaweza kukushauri ukafanye au usiende kufanya na watakutolea mifano ya watu walioshindwa au waliofanikiwa.
Watu hawa wanaweza kukushauri ukafanye au usiende kufanya na watakutolea mifano ya watu walioshindwa au waliofanikiwa.
2. Waliofanya wakashindwa na wameacha.
Watu hawa watakushauri watakwambia kua walifanya wakashindwa na haiwezekani. Sio wote watakwambia usifanye wengine watasema kila mtu na bahati yake.
Watu hawa watakushauri watakwambia kua walifanya wakashindwa na haiwezekani. Sio wote watakwambia usifanye wengine watasema kila mtu na bahati yake.
3. Wanaofanya na wanafanikiwa kwenye hicho kitu.
Hawa pia wanaweza kukushauri na watakushauri kile kitu vyema kabisa kwa kua wanakifanya wao na matokeo wanaona wao.
Wakisema kuna mafanikio ni kweli wameyaona ndio maana wanaendelea kufanya.
Hawa pia wanaweza kukushauri na watakushauri kile kitu vyema kabisa kwa kua wanakifanya wao na matokeo wanaona wao.
Wakisema kuna mafanikio ni kweli wameyaona ndio maana wanaendelea kufanya.
Sasa hapa maamuzi yanakua juu yako kuchagua ni nani wa kukushauri. Siku zote wale unao kaa nao karibu unafanana nao maana watakushirikisha wanavyofanya.
Usiwaangalie walioshindwa kwa kua hata vyuoni, masekondari na shule za msingi watu wanafeli kila mwaka lakini watu hawaachi kupeleka wanafunzi kusoma.
Chagua Wa kumsikiliza. Chagua wa kujifunza kwao.