Maisha yako hayatabadilika kwa kufikiri chanya peke yake,  maisha yako hayatabadilika kwa kufikiri nje ya box peke yake. Maisha yako yataanza kubadilika pale tu utakapoanza kuchukua hatua. Utakapoanza kufanya kwa vitendo vile unavyoviwaza. Utakapoanza kuchukua fursa zinazokujia. Na wakati sahihi ulikua ni jana ila wakati mwingine sahihi zaidi ni leo. Haijilishi muda umeshakupita chukua hatua leo.

Kama tunavyojua mafanikio yana tabia zake. Anza sasa kuziishi na kuzijenga tabia za mafanikio maishani mwako. Tabia hizo zitajengeka kwa kufanya vitendo na matendo yanayojirudia kila wakati hugeuka kua tabia. Tabia hizi haziji ghafla ni muda mrefu. Kutoka kwenye hali uliyonayo sasa hivi kwenda kwa upande wa watu wenye mafanikio makubwa ni kama vita. Ni vita inayopiganwa kati ya hali yako ya zamani,  umaskini, fikra hasi, tabia za umaskini  zote hizo ni tabia ambazo utapambana nazo ili kuziondoa na kua na tabia za mafanikio  fikra chanya, shukrani, upendo na kadhalika.

Huwezi kua kitu ambacho unakichukia hivyo kama wewe ulikua na tabia ya kuwachukia watu wenye pesa namaanisha matajiri, ujue kabisa umechagua kua maskini. Anza leo kuondoa tabia hiyo ya chuki.  Mfano wangu binafsi, mimi nilipokua mdogo nilikua naamini matajiri ni wote ni watu wabaya,  wameiba, wameua, wamedhulumu, wanatuchukia maskini, hivyo nikawa nawaza kuja kuwadhuru nikiwa mkubwa,  ukweli hali hiyo ilinitesa sana nikimwona tajiri na kua na fikra potofu tu juu yake. Ilifika wakati nikiwa sehemu yeyote ambayo kuna watu wenye pesa zaidi yangu hasa wenye magari nilikua nawaza kujilipua. Hali hii ilibadilika pale nilipoanza kusoma vitabu na kufahamu ukweli na ni hatua gani yanipasa kuchukua ili kubadili maisha yangu. Anza sasa inawezekana kabisa kutoka kwenye fikra hzo ulizo nazo na kuanza kuelekea kwenye ili zawadi Mungu aliyoweka ndani yake.

Anza kwa kuuchukia umaskini ukatae katika maisha yako, umaskini unaleta dhambi,  umaskini ni dhambi,  kaa mbali na watu wenye fikra potofu juu ya mafanikio watakupoteza wakimbie kabisa hakikisha neno hata moja halikuingii maana ni kama sumu maneno yao yanaharibu na yatakurudisha kule walipo wao.

Nikupongeze kwa kuweza kusoma Makala hii upo kwenye njia salama anza kuchukua hatua leo.

©Jacob Mushi 2016
Mawasiliano +255654726668 Email jacob@jacobmushi.com.
Chukua Hatua Leo.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading