Coaching

Karibu kwenye huduma ya Coaching. Ninatoa Huduma ya Coaching kwa namna mbili kulingana na mahitaji yako unaweza kuchagua ile ambayo inakufaa.

1. ONLINE COACHING GROUP.

Hili ni kundi la wasap linajulikana kama Usiishie Njiani Academy ambapo unakuwa wewe na wenzako wanaotaka mafanikio makubwa.

Ni program inayokuwezesha mimi kuwa Kocha Wako kwa mwaka mzima.
Ninafuatilia maendeleo yako kila wiki na kila mwezi kwa KaribU sana kuhakikisha malengo yako ya mwaka yanatimia kwa Asilimia kubwa.

Program hii ni ya mwaka mzima na inaendeshwa kwa njia ya mtandao hivyo popote ulipo duniani unaweza kushiriki, inaendeshwa kwa njia ya Kundi la WhatsApp.

Faida utakazopata ukijiunga na Program hii:

1/ Kufuatiliwa Maendeleo Yako kwa Karibu Sana.

Unapata nafasi ya kufuatiliwa maendeleo yako kwa karibu sana hasa kwenye uwekezaji, kuweka akiba, kukuza biashara, hapa utaweza kupewa mbinu za kuvuka changamoto mbalimbali ambazo unakuwa unapitia.

2/ Kuanza Siku Yako Kwa Hamasa Kubwa.

Kila siku asubuhi utapokea jumbe fupi zenye kukuhamasisha na kukupa nguvu mpya ya kuanza siku yako.

3/ Kutengeneza Mtandao Mpya wa Mafanikio.

Unapokuwa kwenye kundi hutakuwa peke yako hivyo basi utakutana na watu tofauti wenye uzoefu kwenye vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwa msaada mkubwa kwako.

4/ Kuwa Karibu na Kocha.

Unapokuwa ndani ya Program hii unapata kipaumbele Zaidi kuliko mtu mwingine ambaye hayupo kwenye kundi. Hii ina maana kwamba ukiwa na tatizo lolote linalohitaji msaada wa kocha utahudumiwa kwa haraka. Ukihitaji ushauri wowote utaupata bure kabisa.

Gharama ya kuingia kwenye Program hii ya ONLINE COACHING ni Tsh 50,000/= (elfu hamsini) na Namba za Malipo ni Tigopesa 0654 726 668 Jina ni Jacob Moshi. Baada ya kufanya malipo nitumie ujumbe wenye Neno KOCHA kwenye WhatsApp namba +255 654 726 668.

2. PERSONAL COACHING

Huduma hii ni maalum kwako wewe ambaye una shida binafsi sana ambayo ungependa nikusaidie kukupa ushauri na njia mbalimbali za kutatua.

Mfano unaweza kuwa unasumbuliwa na tabia ya ulevi wa vitu mbalimbali ambavyo umepambana sana kuacha lakini imeshindikana, mfano ulevi wa pombe, sigara, kubeti, umekuwa na addiction (uraibu) kwenye mapenzi, matumizi mabovu ya pesa, na kadhalika. Haya ni mambo ambayo yamekuwa yanawatesa wengi sana na kuwazuia kabisa kupiga hatua za mafanikio.

Huduma hii ni ya siri na yale ambayo tunafanya pamoja yatakuwa siri siku zote labda wewe mwenyewe uamua kutoa ushuhuda. Huduma hii itakwenda Zaidi ya miezi mitatu kwasababu mwezi mmoja hautoshi kukusaidia kwa haraka, hivyo miezi mitatu kuna baadhi ya matokeo utakuwa umeshaanza kuona kwenye Maisha yako.

Huduma hii inafanyika Online kwa njia ya mtandao, baada ya kulipia utapewa utaratibu mzima namna ambavyo tunafanya kazi pamoja.

Gharama za huduma hii ni Tsh 100,000/= unalipia kwenda namba Tigopesa 0654 726 668 majina ni Jacob Moshi. Ukishalipia tuma neno KOCHA kwenye whatsapp namba 0654 726668.

Karibu Sana Tufanye Kazi Pamoja.

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi