Duniani kuna vitu vingi huwezi kuvipata vyote huwezi kuvijua vyote ufanyeje? Soma hapa….

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Habari ya leo ndugu msomaji  wetu. Ni matumaini yangu mnaendelea vyema  na maishz yenu. Karibu tena leo kwa kujifunza pamoja. Kwani mafanikio yetu ni mafanikio yako.

Duniani kuna vitu vingi sana vya kuvutia vingine vya ajabu vya kutisha n.k. Pia kuna watu wa aina mbalimbali na tamaduni za namna mbalimbali.  Pia kuna vipaji vya aina mbalimbali. Ujuzi wa aina mbalimbali elimu nyingi sana.
Huwezi kuvifahamu vyote hata nusu huwezi.  Hata ukijitahidi vipi hutaweza kwanza muda hautoshi kujua vyote vingine inabidi ubaki kuvisikia tu.

Kuna magari mengi ya aina mbalimbali. Huwezi kuwa nayo yote. Kuna simu nyingi za aina nyingi huwezi kua nazo.  Kuna vingi vingi sana siwezi kuvitaja hapa wewe chagua unachokipenda na uangalie uwezo wako wa kukifikia

Unachotakiwa kufanya ni kutafuta kimoja cha kufanya na cha kukifahamu kitakacholeta manufaa kwenye maisha yako. Vingine achana navyo wewe visikie tu maana hata ujitahidi vipi hutaweza kufahamu vyote. Jikubali kwa kile unachokifanya kwa kipaji ulichonacho eka juhudi usikate tamaa mpaka uuone mwisho.

Katika maisha kuna vikwazo vingi sana. Kuna changamoto nyingi sana. Kitu cha muhimu ni kuchukulia changamoto kama mafunzo ya kufika kule tuendako. Usiogope, Usiogope, Usiogope.

Hua ninapenda kusema kuwa haijalishi  mpaka sasa hujafanya nini. Haijalishi una umri gani. Wewe angalia sababu moja tu “uko hai na unazo nguvu za kufanya mabadiliko” yako mambo mengi sana kama nilivyoyataja tena sijamaliza hata nusu sijafika. Wewe chagua ukipendacho ukifanye. Uhai ulionao sasa ni wa thamani sana utumie vizuri kwani wakati unasoms hapa kuna mgonjwa hospitali hawezi chochote. Kuna wengine wanakata roho sasa hivi. Kuna wengine ni vipofu hawajaweza kusoma kama wewe hii ni nafasi ya pekee sana uliyonayo itumie vizuri. Pia ninajua kuna wengine hawana mikono au vidole vya kuandika hichi nilichoandika hvyo sitachoka kuandika ili wewe ulie na macho na nguvu usome.

Mungu akubariki akulinde akufanikisha malengo yako yote.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

Mwandishi  Kocha wa Mafanikio na Mjasiriamali.

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading