Kila kitu kina misingi na kanuni zake, maisha nayo yana misingi na kanuni zake. Ili uweze kuishi na kufurahia maisha katika kiwango cha juu unatakiwa kufahamu na kuishi misingi na kanuni.

Hizi ni ambazo nimezifanya ziwe kama mwongozo wako.

AFYA:

Afya ya Mwili. Afya ya Akili. Afya ya Kiroho. Vitu Hivi vitatu ni muhimu sana kwenye maisha yako. Huwezi kusema una maisha bora kama hizi sehemu tatu hazina ubora au hazina afya.Unapaswa kuwa na mikakati ya kufanyia kazi sehemu hizi kwasababu ndio zimebeba maisha yako yote

HEKIMA:

Wakati Sahihi wa Kukaa Kimya. Wakati Sahihi wa KuongeaKitu Sahihi Cha Kuongea. Hii itakuwezesha uweze kuishi na wengine vizuri. Kuna watu wenye tabia mbalimbali zinazokera bila ya Hekima utakuwa mtu mwenye hasira, chuki na Visasi hutaweza kufurahia maisha.

UTAJIRI:

Uwekezaji, Mali, Mtandao wa Watu, Upendo.Maisha ili yawe bora ni lazima ufikie kile kiwango ambacho Hutakuwa na Matatizo yanayoletwa na ukosefu wa pesa.Hivyo ni muhimu kuhakikisha vile ambavyo unatakiwa kuvifanyia kazi ili kujenga mifereji ya kipato ambayo inadumu.
Huwezi kuvipata hivyo pasipo na maarifa Sahihi, kuwa na malengo, kuchukua hatua kubwa, kutokuishia njiani.
Yakupasa uwe mvumilivu, usiwe mtu wa kuyumbishwa na yale yanayotokea bali uwe mtu unaesimamia misingi ya kile unachokiamini.Karibu Sana Rafiki katika safari ya kutengeneza Maisha bora.

Nakutakia Kila la Kheri.

Rafiki yako Jacob Mushi.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading