Ili uweze kuwa na mwili wenye afya bora lazima ule vyakula bora na kufanya mazoezi. Vilevile kwenye akili yako ni vyema ukapata maarifa ambayo yanakufanya uwe na ufahamu bora. Watu wenye uwezo sana ukiacha wale ambao wana uwezo wa kipekee toka wanazaliwa wengi wanaongeza uwezo wao kwa kusoma vitabu.
Soma Kitabu: SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO
Sasa kwenye kusoma vitabu kunazingatia wewe ni nani, unataka kuwa nani. Huwezi kusoma tu kila kinachoitwa kitabu. Kwenye mwili kama unataka kutengeneza misuli huwezi kula vyakula anavyokula mtu anaetengeneza mwili wake kwa ajili ya mitindo. Maarifa unayotafuta kwenye vitabu yanatakiwa yaendane na kusudi na maono yako. Hii itakuwezesha ukue vizuri katika kile kitu ambacho unataka kuja kuwa.
Unakua Kiufahamu.
Hii ipo wazi kabisa, ukiwasimamisha watu wawili msomaji wa vitabu na asiyesoma vitabu kabisa au anaesoma vitabu vya hadithi utaweza kuona utofauti wao hata katika kujieleza tu. Mara nyingi wasio soma vitabu wanakuwa waoga kwasababu kichwani kunakuwa hakuna kitu.
Ukitaka kuongezeka kichwani tafuta vitabu mbalimbali vya maarifa hata visivyo vya fani yako usome ili ukue.
Unapata Uwezo Wa Kutatua Matatizo.
Msomaji wa vitabu anakuwa na uwezo mkubwa wa kutatua matatizo kwasababu kuna njia nyingi amezipata kwenye vitabu. Linapokuja swala la tatizo msomaji wa vitabu anakuwa na uwezo wa kuliona tatizo katika kona nyingi Zaidi.
Changamoto nyingi tunazoziona ni kubwa inasababishwa na udogo wetu wa akili. Unaliona tatizo kulingana na uwezo wako wa akili ulivyo. Kuna jambo linaweza kutokea kwa mtu akapata hadi presha wakati huo huo linatokea kwa mtu mwingine na anakuwa kawaida kabisa.
Unapata Uwezo wa Kuona Mbali.
Kwenye vitabu tunaona mawazo ambayo hayajawahi kuwazwa huku duniani. Kuna mambo mengi yamewekwa kwenye vitabu ambayo hakuna mtu angeweza kuyawaza kwasababu yalipitia kwa mtu huyo pekee. Kama utaweza kusoma vitabu utakutana na mawazo ambayo yatakufungua ufahamu wako na utaweza kuona mbali kwenye yale unayoyafanya.
Unaongeza Uwezo wa Kuziona Fursa.
Unaweza kwenda kwenye jamii ambayo inalalamika sana hali ni ngumu lakini kwasababu umeweza kukuza ufahamu wako utajikuta unaona fursa zimewazunguka. Tukija kwenye jambo ambalo unalifanyia kazi unakuwa unapata uwezo wa kuona njia mbalimbali za kufanikiwa.
Kwa kusoma vitabu unaweza kujikuta unaona fursa nyingi hasa kwneye zile changamoto ambazo unapitia kila siku.
Unakuwa Tofauti Kabisa na Wasio Soma Vitabu.
Unakuwa tofauti katika mazungumzo yako, huwezi kuwa mtu anaongea ongea hovyo.
Namna unavyowachukulia wengine, namna unavyoyaelewa Maisha namna unavyoishi inakuwa ni tofauti kabisa. Unakuwa ni mtu ambaye amejitambua. Unakuwa sawa na mtu ambaye anasafiri duniani, hii ni kwasababu unatembea kwenye akili za watu kwa kupitia yale ambayo wameandika.
Zipo faida nyingi sana ambazo kila mmoja anaweza kutaja kulingana na yale ambayo vitabu vimemfanyia. Unaweza kuzitaja pia mwishoni mwa Makala hii,
Soma vitabu Ukue Kiakili.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/