Hatuishi mara mbili duniani, ukishaondoka umeondoka. Katika vitu muhimu sana vya kufanya unapofanya chochote ni kukifanya kama hutakaa uje ufanye tena.

Kama umekutana na mtu mjali kama vile ndio mara yako ya mwisho hamtakaa muonane tena.
Umekutana na fursa ifanye kama vile ndio haitakaa irudi tena.

Onyesha upendo wako wote kwa wengine kama ndio mwisho wako leo.
Kama ni kufurahi furahi ipasavyo kama ndio mwisho wa kufurahi leo.

SOMA: WEWE NI MSHINDI

Kwanini ufanye yote hayo?
Hakuna ajuae kesho, wako walioweka mipango mingi na mizuri sana. Wapo pia waliokua na ndoto kubwa mno lakini Ghafla tunasikia hatuko nao tena duniani.

Unapokutana na fursa yeyote ile ikaingia mikononi mwako, ifanye kwa uwezo wako wote. Maana hujui kama ndio ya mwisho hiyo.
Nafasi ya Pekee uliyonayo ya kubadilisha maisha yako ni leo sio siku nyingine yeyote.
Kama kuna jambo unatamani kulifanya maishani mwako, tafadhali anza leo usiseme ipo siku nitaanza, mara ooh! Najipanga! Nani amekupa hiyo siri kwamba utakuwepo hadi mipango yako ikamilike? Anza leo fanya kwa bidii zote, uwezo wote, akili zote na utaleta mabadiliko kwenye dunia na maisha yako.

Ipo siku utakua huna nguvu ulizo nazo sasa. Utasema ningejua ningefanya hivi. Ningejua nisingefanya vile! Leo ndio una nafasi ya kubadilisha!

Chochote unachokifanya sasa kifanye kama hutakaa upate nafasi tena.
Kufahamu mengi zaidi soma kitabu changu Siri 7 za Kuwa Hai Leo

Karibu sana
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading