Connect with us

USIISHIE NJIANI

Fanya maamuzi.

 Tatizo kubwa tulilonalo hapa nchini sio pesa. Tatizo kubwa tuna watu wengi ambao ni waoga kufanya maamuzi. Mtu anakutana na fursa nyingi anahamasika Lakini tatizo lipo kwenye kuchukua hatua. Upo hivyo ulivyo leo kwa sababu ya maamuzi uliyoyafanya siku za nyuma pia vile vile upo vile ulivyo haujaendelea, kwa sababu ya woga uliogopa Kufanya maamuzi […]

 Tatizo kubwa tulilonalo hapa nchini sio pesa. Tatizo kubwa tuna watu wengi ambao ni waoga kufanya maamuzi. Mtu anakutana na fursa nyingi anahamasika Lakini tatizo lipo kwenye kuchukua hatua.

Upo hivyo ulivyo leo kwa sababu ya maamuzi uliyoyafanya siku za nyuma pia vile vile upo vile ulivyo haujaendelea, kwa sababu ya woga uliogopa Kufanya maamuzi juu ya fursa uliyokutana nayo.

Maisha yako yaanza kubadilika pale tu utakapoanza kuchukua maamuzi sahihi juu ya fursa mbalimbali zinazokuzunguka na unazokutana nazo kila siku. Acha woga hakuna kisichowezekana hata wewe unaweza kufanya mambo makubwa na ukaacha historia hapa duniani kabla hujaondoka,  wapo Vijana wadogo wanaozungumziwa kila siku na bado hata hawamaliza safari kwanini usianze na wewe leo.?

 Ni wakati wa kufanya maamuzi sasa kama kila siku unapanga mambo na hayatokei unarudi pale pale ulipo, fanya maamuzi leo, woga ni adui yako wa kwanza anza kumkataa huyo adu kwanza.
 Pia usiishie kufanya maamuzi tu anza safari pambana hadi jasho la mwisho hadi upate kile unachokitaka.

Ni wakati wako acha kusita sita muda unakwenda una masaa 24 tu unayoyachezea kila siku na ndio hayo hayo wanayotumia wenzako na wamekua mabilionea.

Twende tukaipindue dunia.
Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016 Tuandikie 0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in USIISHIE NJIANI

To Top