SOMO: ILINDE NDOTO
Ndoto ni nini? Ndoto ambayo tunakwenda kuizungumzia sio ndoto unayoota ukiwa umelala. Ni ndoto ya mchana ni  kile kitu unachotamani kuja kukipata siku moja kabla hujaondoka duniani Ndoto inaweza kua katika makundi ya aina mbalimbali, unaweza kua na ndoto ya kua Rais, Mwimbaji bora, Mchezaji bora, Mwandishi Bora, Mfanyabiashara maarufu.
Vile vile unaweza kua na ndoto ya kumiliki vitu, nyumba nzuri ya kifahari sana labda ya milioni 300, Gari la kifahari sana, Unaweza kua na ndoto ya kumiliki utajiri au kua Bilionea. Kutembelea nchi fulani na kadhalika.
Zote hizo ni ndoto ambazo kila mmoja alikua nazo huenda ni kipindi anakua ua hata sasa bado anayo. kwa bahati mbaya sana watu wengi wamekua na ndoto kubwa sana wakiwa wadogo na kuzipoteza walipoanza kuingia kwenye uhalisia wa maisha

 

VITU VINAVYOWEZA KUIPOTEZA NDOTO YAKO.
Ugumu wa Maisha.
 Maisha yanavyozidi kubadilika na kua magumu ndipo baadhi ya watu huanza kuasahu vile vitu ambavyo walikua  wanatamani waje kua navyo. Maisha yanapokua magumu sana wengi huona haiwezekani tena wao kufikia ndoto zao hivyo kukata tamaa kabisa na kuamua kua na maisha ya kawaida. Mtu anaweza kujitazama vile alivyo na kuona yeye hafananii kabisa kuja kua Rais wa nchi hii labda kutokana na familia aliyotokea au maisha yanayoendelea sasa hivi.Nakuomba kama unapitia hali hiyo anza kuikataa kabisa ili usije kupotea.
Marafiki wabaya.
Marafiki na watu unakua nao mara kwa mara wanaweza kua sababu kubwa sana kukupoteza kabisa na kukufanya wewe uache kupigania ndoto yako. Ndoto yako ni ya thamani sana ndio maana inapata upinzani. Ndio maana uutaambiwa haiwezekani. Ndio maana watakucheka ukiwaambia wewe unataka kua Rais wa nchi hii. Au unataka kua Bilionea. Mara zote watu wanakuhukumu kutokana na hali uliyonayo sasa hivi. Unaweza kuachwa na Mpenzi wako umpendaye kwa sababu tu yeye anaangalia maisha uliyonayo sasa hivi na hata ukimueleza ndoto zako haamini kutokana na hali yako ya maisha uliyonayo sasa.
Ufanyeje?
Kaa nao mbali wale watu ambao hawana ndoto kama za kwako. Kaa mbali na watu ambao wanafikiri kama kuku. Yaani wao wamejiona kwamba ni maskini na haiwezekani kua tajiri labda kuiba tu. Inawezekana ni watu wako wa karibu sana labda kaka, dada, wazazi  ufanyeje? usikubali kuwasikiliza weka pamba sikioni. Mimi kuna mtu aliniambiaga hizo ni ndoto za mchana haziwezi kutokea kamwe lakini sijakata tamaa naendelea kufanyia kazi ndoto zangu.
UNALINDAJE NDOTO YAKO?
Iandike.
Kama unasema una ndoto lakini bado ipo kichwani bado hujaelewa maana yake. Katafute Notebook nzuri sana ya gharama Huwezi kuandika ndoto ya kua Bilionae kwenye note book ya elfu mbili aisee?? Tafuta notebook ya Gharama hata ya 20,000 ili uweze kuitunza vizuri. Andika kila kitu unachokitaka kwenye dunia hii. Hakikisha umeandika kila Kitu na usiache hata kimoja.
Hii ni njia ya kwanza ya kuilinda ndoto  yako. Nikikutana na wewe sehemu  Uniambie au unionyeshe kilipo kitabu chako cha ndoto. Andika ni Jinsi gani unaweza kupata vile vitu. Ni ujuzi wa namna gani unahitaji ili uweze kufikia ndoto zako. Ni watu wa namna gani unahitaji kuambatana nao ili ufanikiwe kwenye doto zako. Andika ni Baada ya Muda gani utakua umefikia Ndoto zako sasa hapa Ni somo jingine kabisa jinsi ya kuandika malengo. Malengo ya muda mfupi na Muda mrefu. 
Soma ndoto zako kila siku
Asubuhi na kabla ya Kulala. Soma kila siku namaanisha kila siku asubuhi na jioni. Kwanini usome kila siku ? Unaichora au unaiingiza picha ya ndoto zako ndani ya ubongo wako hii itakufanya chochote utakachokutana nacho kama hakiendani na ndoto yako uweze kukiepuka na  kama kinaendana basi uweze kukivuta.  Unaposoma inajijenga kwenye akili yako na kutengeneza ukaribu wa wewe kuifikia zaidi.  Soma na tafakari.
Tenga Muda peke yako.
Hakikisha unatenga Muda wa peke yako angalau kila wiki ukiwa peke yako sehemu ambayo haina usumbufu wowote. Sehemu hiyo utakua unaipa akili yako nafasi ya kutafakari juu yako wewe. Jitazame ulivyo sasa halafu jitazame wewe ukiwa umefikia kwenye ile ndoto yako. Kama ni gari basi anza kujiona jinsi unavyoliendesha lile gari la ndoto yako. Kama ni Rais embu jione ukiwa Ikulu basi Jione ukiongoza majeshi. Kama ni Bilionea anza kuona ukiwa Bilionea utakavyokua. Utakavyoweza kubadilisha maisha ya watu wengi sana Duniani. Ona jinsi dunia inavyofurahia Mungu Kukuumba wewe kwasababu maisha yao yamebadilika. Nashauri hili ufanye angalau lisaa limoja ukiwa peke yako bila simu wala kifaa chochote cha mawasiliano.
Soma Vitabu na Fanyia Kazi ndoto yako Kila siku.
Soma vitabu ambavyo vitakuza ufahamu wako ili wewe uweze kuifkia ndoto yako. Kama unataka kua Rais wa Nchi lazima ujue kua unakwenda kuongoza watu hvyo bi vitabu gani usome ile ukuze ufahamu wako. Unataka kua Bilionea hutaweza kua bilionea na ufahamu ulionao sasa hivi mali zote zinatakiwa ziongozwe na wewe hivyo jijengee tabia ya kujisomea vitu mbalimbali juu ya ile ndoto yako.  Ili ufikie Ubilionea unaanza na hatua moja anza leo kupiga hatua moja moja hadi ufikie kule unakotaka. Usikubali kabisa siku ipite ujafanya chochote juu ya Ndoto yako ni kupoteza fursa.
Kama tunavyojua fursa ya kwanza ni uhai tulionao leo hivyo usitumie vibaya leo siku zote unakuaga na leo tu. Ukiweza kuipangilia leo vizuri itakufikisha kwenye ndoto yako.
Jipongeze
Kwenye kila hatua unayopiga jipongeze ili kujiongezea hamasa na wewe uweze kusonga mbele. Unaweza kujipa zawadi ndogo ndogo ambazo hua unazipenda kila unapopiga hatua kuelekea kule unapotaka.
Iseme ndoto yako sehemu yeyote unapokua.
Kwanini uiseme kwasababu una Imani na Imani ni kua na hakika juu ya mambo yasiyoonekana. Hata Yusuf alianza kuwaambia ndugu zake kwamba anaona ndoto anaona akiwaongoza. Walimkemea lakini hakusita kuendelea kuwaambia. Hii itakusaidia unapokamilisha iwe ushuhuuda kwamba huyu jamaa alituambiaga anakuja kua Rais, Bilionea, Mtu mkuu sana.
Huwezi kuitwa mchawi au Freemason kama umeanza kusema sasa hivi  wakati huna kitu kwamba utajenga Ghorofa au utamiliki BMW. Atakae kusema atakua hakujui kabisa. Walewale wanaokukatisha Tamaa ndio watu wakuwaimbia ile ndoto yako.HAta wakikusema wewe endelea kuisema. Unapoisema inakupa ujasiri wa kuendelea mbele bila kukata tamaa.
 
Naamini unakwenda kuilinda ndoto yako. na kuifanyia kazi ili Itimie.
Asanteni sana na Karibu sana.
Jacob Mushi

One Response

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading