Fanya tena

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read

Matokeo ya kile unachokifanya yanaweza yasitokee kama ulivyotarajia au kupanga haimaanishi kwamba unachokifanya sio sahihi.  Kuna kua na sababu nyingi za kile ulichofanya kinapokuja na matokeo tofauti. Inawezekana wewe ndie mwenye tatizo. Kabla hujaamua kuacha kufanya au kutafuta njia nyingine kaa chini utafakari ili ufahamu chanzo halisi cha tatizo.

Watu wengi hukata tamaa haraka sana pale ambapo alitarajia apate faida kwenye biashara mpya aliyoianza badala yake akapata hasara na ni kwa mara ya kwanza ni kweli inauma lakini kitu chochote chenye thamani kinahitaji uvumilivu. Kinahitaji wewe kua na moyo mkuu. Kitu kikubwa cha kufanya matokeo yapokuja tofauti sio kuacha kufanya ni kujifunza zaidi ongeza maarifa zaidi kwenye kile unachokifanya.

Fanya tena. Unaweza kujiuliza. Kama kitu sioni matokeo nikifanye mara ngapi mimi nitakwambia rudia hata mara kumi na huku ukiwa unajifunza zaidi usipoona matokeo ndio uache.

Kabla hujakata tamaa jiulize umefeli mara ngapi? Kwanini umefeli tatizo ni wewe au ni kile unachokifanya?  Unaweza ukasingizia biashara ngumu kumbe wewe ndie mgumu huelewi na hujifunzi. Kama kitu hicho unachokifanya wengine wanafanya na wanafanikiwa tatizo halipo kwenye hicho kitu tatizo lipo kwako anza kujitibu wewe kabla hujatafuta njia nyingine.

Atakaevumilia mpaka mwisho ndie atakaeyaona matunda ya uvumilivu wake. Usikate tamaa maana wako wenzako walishapita hapo unapopita wewe usiogope maana haupo mwenyewe. Kaa na waliofanya hio biashara na wakafanikiwa watakushauri vizuri zaidi.

FANYA, FANYA, FANYA,……  hadi uone matokeo unayoyataka.

Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie 0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading