“Knowing Is Not Enough; We Must Apply. Wishing Is Not Enough; We Must Do.”- Johann Wolfgang Von Goethe

Kujua tu haitoshi lazima tuingize kwenye vitendo yale tunayojifunza na kujua,  kutamani tu haitoshi tuchukue hatua kufikia vile vitu tunavyotamani.

Kua na ndoto kubwa haitoshi  inatakiwa ujue kuingia kwenye vitendo, vitendo siku zote ndio vinaleta matokeo.

Vikwazo utakutana navyo lakini visiwe sababu ya wewe kuacha bali sababu ya wewe kukua na kukomaa.
 Anza leo kufanyia kazi yale unayojifunza hapa kila siku maana haitafaa ujifunze tu peke yake maisha yako yanatakiwa yabadilike utoke sehemu uliyokuwepo na usogee mbele zaidi na hili ndilo dhumuni kuu  la maisha kuendelea. Kama unachokifanya hakiendelei ni tatizo hilo.

Unapozaa mtoto akawa hakui akabakia kutambaa tuu miaka kadhaa huwezi kufurahia lazima umkimbize kwa daktari akafanyiwe uchunguzi. Vivyo hivyo katika maisha yetu kila siku kama husogei maana yake ni upo kwenye matatizo makubwa unahitaji tiba ya akili. Unahitaji kushauriwa ili uweze kusogea mbele.

Lengo la mimi kukuandikia makala hizi katika blog hii ni wewe usome ujifunze ufanyie kazi na maisha yako yaweze kubadilika na kama huoni mabadiliko ujue kuna tatizo mahali unitafute tuongeee zaidi au uache tu kusoma maana kama hubadiliki itakua haina maana ya wewe kuendelea kusoma.

Maisha yako ni lazima yawe na mabadiliko chanya japokua unapitia changamoto mbalimbali lakini mabadiliko chanya lazima yawe yanaonekana. Hilo ni la muhimu sana kwenye maisha yako rafiki yangu.

Nakutakia wakati mwema.
Jacob Mushi
0654726668
jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading