FUNGUO: TAARIFA.

jacobmushi
2 Min Read
Habari za siku ya leo Rafiki natumaini unaendelea vyema.
Leo kwenye kipengele cha funguo tunaangalia kitu kinaitwa taarifa.

Taarifa ni zile habari au maelezo unayoyapokea. Zipo njia mbalimbali za mtu kupokea taarifa kwa kipindi hiki njia zimekua rahisi sana. Kwa kupitia simu yako ya mkononi unaweza kupokea taarifa za aina zote, kwa picha, kwa sauti, au hata video. Mara nyingi taarifa zinazosambazwa zinakua ni taarifa hasi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
Taarifa hizi zinapikua hasi zinaufanya ubongo wetu kuzipokea kama tahadhari hivyo wakati mwingine kutufanya tushindwe kufanya mambo mengine.

Kama wewe taarifa unazozipokea kila siku ni hasi utajikuta mambo yako hayaendi. Sio kwamba kuna mchawi lah! Ni taarifa hasi zimeufanyav ubongo wako kuacha kufikiri mambo mengine ukaweka tahadhari. Chunga sana taarifa unazopokea kwenye ubongo wako. Mfano sasa hivi tuna taarifa nyingi juu ya uchumi kuyumba na hali mbaya ya kifedha iliyopo nchini. Ukweli ni kwamba kinachofanya hali hii kuwa mbaya zaidi ni watu kuzidi kupokea taarifav hizi. Badala ya watu kutafuta suluhisho akili zao zinawaambia hali ya uchumi ni mbaya kila mahali. Sasa jiulize kama kila akili ya MTANZANIA itasema hivyo tutakua na mabadiliko?

Taarifa yeyote hasi kwenye ubongo wako inaufanya ubongo wako kuweka tahadhari. Vile vile taarifa hizi zinajenga tabia ya woga juu ya mambo fulani katika maisha. Hivyo utajikuta unashindwa kufanya mambo ya muhimu kwasababu ya woga.

Ukitaka kuwa na maisha ya furaha na maendeleo, punguza au badilisha kabisa chanzo cha taarifa.  Kuna watu huwa hawasafiri kabisa mwishoni mwa mwaka kisa walisikia au waliambia kunatokeaga ajali sana.  Kuna mambo mengi sana ukichunguza maishani mwako unaogopa tu kuyafanya kwakuwa ulisikia taarifa mbaya juu yake.

Badili leo chanzo cha taarifa  zako. Maisha yako yatabadilika.

Jipatie kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo.

Jacob Mushi
Mwandishi, Mjasiriamali, na Mhamasishaji.

0654726668
ushauri@jacobmushi.com
Tembelea www.jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading