Habari za Leo rafiki na msomaji wa Blog hii. Natumaini wewe ni mzima kiafya, na pia unaendelea vyema katika mapambano ya kuboresha maisha yako. Tunakwenda kuona leo katika kipengele cha funguo, aina ya ufunguo wa kufanya maisha yako yasonge mbele. Kuna vitu vingi tunafanya bila kujua au kwa kujua na vinakua sababu ya sisi kukwama.

Inawezekana wewe umekua mkosoaji wa kila kazi wanazofanya wengine. Hushauri pia hutoi maoni ambayo yatamfanya mwenzako asongee mbele. Badala yake maneno yako siku zote yanarudisha wengine nyuma. Huo ni mlango ambao unakufungia wewe kusonga mbele.

Mara nyingi nimekua naona watu wengi wakiwa wakosoaji wakubwa wa kazi za Watanzania wenzao. Wengi tunawaona wenzetu hawawezi hata siku moja badala yake tunaona wanaoweza ni watu weupe peke yao. Unakutana na mtu anasema, “Hapa Tanzania sijaona waigizaji kabisa siwezi kupoteza muda kutazama filamu za Kitanzania” au “Bidhaa nyingi za Tanzania ni feki” au mtu anakwambia hicho unachokifanya unapoteza muda. Ukimuuliza ana ushauri gani kwenye hayo anayoyakosoa ili yawe bora unakuta hana mchango wowote. Haiwezekani uone makosa halafu ukose suluhisho. Ukiwa na uwezo wa kuona makosa katika jambo fulani lazima uwe na suluhisho lake. La sivyo bora uache kukosoa kama huwezi kushauri au kutoa maoni.

Hakuna mtu aliwahi kuanza akiwa vizuri asilimia mia moja hivyo chochote kinachoanza lazima kiwe na mapungufu yake. Unapoona mapungufu katika   bidhaa au huduma ya mwenzako njia bora ya kumsadia ni kumshauri. Kama mtu hapokei ushauri huyo na yeye ni tatizo. Lakini ukishashauri umemaliza kazi ni juu yake kufanyia kazi.
Funguo ya kukuwezesha wewe uweze kupiga hatua kwenye kile unachokifanya ni kukubali wanayofanya wengine. Anza kuonyesha kwamba unajali na kuthamini mchango wa wengine katika jamii yako. Hakuna atakaejali unachokijua kama wewe hujali kile anachokifanya.

Jijengee tabia ya kukubali vitu vya wengine ili na wewe uweze kukubaliwa katika kile unachokifanya. Amua leo kutumia ufunguo huu ili uweze kupiga hatua kwenye maisha yako. 

Jipatie Kitabu SIRI 7 ZA KUWA HAI LEO 


Success Kingdom
Jacob Mushi
Mjasiriamali, Mwandishi, Mwalimu na Mhamasishaji
Website; www.jacobmushi.com
Email; ushauri@jacobmushi.com
Phone; +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading