FUNGUO.

Funguo kazi yake kuu ni kufungua na kufunga. Popote kwenye vitu vya thamani kunakua kumefungwa na ulinzi wa kutosha.
Mmiliki peke yake ndio hua na ufunguo. Yeyote anaengia lazima awe na ruhusa kutoka kwa mmliki wa sehemu hiyo.
 
Ili uweze kusogea mbele ufungue milango ya fursa na kila aina ya kitu kizuri unachokihitaji unahitaji funguo.
Funguo ndio zinatuwezesha kuingia ndani, bila funguo huwezi kuingia ndani, ukiona umefunguliwa ukaingia ujue huna mamlaka mahali hapo.
Hata kama kuna vitu vizuri ndani hutaweza kufanya maamuzi utagawiwa kiasi kidogo tena baada ya kuomba.
 
Ni vyema sana na wewe uwe na ufunguo wako umiliki vyumba chako vilivyojaa mambo mbalimbali.
Unapataje funguo zako?
Kwenye mafanikio pia unahitaji funguo za kukuwezesha kufungua yale mambo unayoyahitaji,
 
Funguo za mafanikio zipo za aina nyingi sana, leo ninakupa funguo mmoja ambao hua nakupatia kila siku.
 
Ufunguo wa kwanza ninao kupa mimi ni maarifa, maarifa yanakuwezesha wewe kufungua mambo mengi sana na kuweza kufikia mambo makubwa.
Endelea kuwepo hapoa ujifunze aina mbali mbali za funguo zikuwezeshe kufika mambo.
Ukimiliki funguo unakua jasiri maana unaweza kufungua na kuingia popote.
 
 Karibu sana Rafiki,
Jacob Mushi
This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *