Habari za leo ndugu msomaji wa blog yetu. Ni matumaini yangu unaendelea vizuri katika maisha yako. Tunakuombea Mungu ufanikiwe.

Leo tunangalia vitu vya kufanya  ili uweze kuendelea kufanya mambo na ufanikiwe ” ISIPITE SIKU HATA MOJA HUJAONGEZA THAMANI YAKO”  Katika maisha yako jitahidi siku nzima isipite hujafanya mambo haya yaani ili kuongeza thamani yako kwako na kwa watu wanaokuzunguka inakubidi ujitengenezee utaratibu wa kujifunza kitu kipya kila siku. Unapokua unajifunza vitu vipya ufahamu wako dhidi ya mambo unakua ni mpana zaidi. Yapo mambo mengi sana ya kujifunza kila siku mojawapo ni kusoma makala kama hizi zetu zinazojenga na kukuinua kiroho na kimwili. Soma vitabu vya dini soma sikiliza audio za kuhamasisha utaendelea kukua kiufahama na maarifa kila siku hiyo itakupa uwezo wa kutatua matatizo yanayokukabili na matatizo ya wengine.

Jitahidi isipite siku moja hujatatua changamoto yeyote iwe inakuhusu au haikuhusu. Dunia imejaa watu wenye matatizi mengi jitahidi uwe unajihusisha katika kuwasaidia wengine kusuluhisha matatizo yao kama tulivyoona kwenye makala iliyopita ukiondoka unaacha alama gani duniani? Hiyo itakua ni moja ya alama unayoiacha. Wasaidia watu kutatua changamoto zao japo kwa kuwashauri hawatakusahau daima. Pia hiyo ni njia ya kukua kiufahamu.

Jambo lingine hakikisha isipite siku hujamweleza mtu habari njema itakayomsaidia katika maisha yake. Kwenye mitandao ya kijamii eleza unachokijua kuna ambaye kitamsaidia. Unapoongea maneno mabovu habari mbaya sidhani kama kuna mtu atakukumbuka. Unapoongeza thamani kwenye maisha ya watu  kuna siku utapita mtaani utashangaa wanasema huyu mtu namfahamu. Ivi utajisikiaje ukikumbukwa kwa mambo mabaya uliofanyia wengine. Jitahidi ukumbukwe kwa mema kua Mjumbe wa habari njema zinazoinua na kuwasaidia wengine hii itaongeza thamani yako katika jamii pia ni mojawapo ya njia ya kuacha alama duniani.

Ninashukuru kwa kua mfuatiliaji wa makala zetu Mungu akubariki sana. Ninafurahi sana ninapopokea ujumbe kwa watu kua makala zetu ni nzuri. Tutajitahidi tuongeze ziwe bora zaidi ziwasaidia na wengine unaweza kushare makala hii kwa wote uwapendao utakua umesambaza habari njema. Wasiliana nasi kwa 0654726668 au e-mail riseshine500@gmail.com.
Asante ubarikiwe sana

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading