400: Hakuna AnaeKulazimisha.

jacobmushi
2 Min Read

Ulipokuwa mtoto kuna nyakati ulikuwa ukichelewa kuamka unakuja kuamshwa na viboko au wakati mwingine unamwagiwa maji. Kuna wakati pia ulikuwa unalazimishwa kusoma kwa bidii na unaambiwa uweke maji kwenye beseni ili usisinzie.

Naomba ujiulize hivi sasa ni nani tena anaekulazamisha tena ufanye kazi kwa bidii ili uwe na pesa? Ni nani tena anaekuja kukuamsha mapema ili uwahi kwenye majukumu yako? Ni nani anaekuambia uchelewe kulala ili uweze kufanya mambo mengine ya ziada? Ukweli ni kwamba hakuna tena mtu wa aina hiyo. Sio Watoto wako, sio mke wako na wala sio mume wako.

Hakuna mtu atakuja tena akushike akuvute uende ukafanye majukumu yako. Ambaye amebaki na wewe ni wewe mwenyewe, ambaye anakuona vizuri na kukufuatilia kuliko mwingine ni wewe mwenyewe. Hakuna mtu mwingine anaejali unachokifanya kama wewe. Nikwambie ukweli Rafiki hata ukifa leo ni wachache sana watajali kuhusu uwepo wako hapa duniani, labda tu Maisha yako uwe uliyatoa vya kutosha kwa ajili ya wengine.

Usipoamua kujilamisha wewe mwenyewe hakuna atakaekuja kukulazimisha tena. Hata ukiacha unachokifanya sasa hivi watu wachache sana wataumia na baada ya muda watapata mtu mwingine mpya. Hapo ulipoajiriwa ikitokea bahati mbaya umekufa leo haitachukua muda atapatikana mtu mwingine wa kuchukua nafasi yako.

Hivyo Rafiki yangu wewe ukishindwa kujithamini nna kujilazimisha uwe bora kila siku na uwe na maendeleo hakuna mtu mwingine anaejali. Watu wengi wanajali wanapata nini kwako kuliko kile wewe unachokipata. Hivyo ili uweze kuwaepuka watu hawa unapaswa kuwa bora sana ili uwavutie watu sahihi.

Unapaswa kuamua mwenyewe na ujilazimishe wewe mwenyewe kufanya hata vile ambavyo mwili wako unakataa lakini ni vitu vinavyoleta maendeleo. Ukiendelea kufanya kile unachokifanya kila siku utaendelea kupata matokeo yale yale.

Ukweli mimi pia sikulazimishi, ninachofanya ni kukupa maarifa sahihi wewe ndio utaamua uchukue hatua au uyaache. Maamuzi utakayofanya ndio yataamua uwe wapi kesho. Ulilazimishwa kipindi kile ambacho ulikuwa upo chini ya wazazi sasa hivi kitu mtu anaweza kufanya ni kukushauri tu.

Usiache kujiunga nami kwa Huduma ya Coaching >>>> https://jacobmushi.com/kocha/

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading