Habari ya Asubuhi Rafiki, Napenda leo kufahamu ni kitu gani kinakufanya wewe ubakie katika hali ile ile bila mabadiliko! Unafikiri ni nani atakua anahusika katika kufanya wewe ukwame? Ukweli ni kwamba hakuna mtu mwingine ila ni wewe peke yako. Wewe ndio sababu ya kuwepo hapo ulipo sasa. Inawezekana upo hapo ulipo kwasababu ya matokeo mazuri uliyoyapata huko nyuma aua kwasababu ya kukwama kutokana na changamoto unazopitia. Unaweza kubadiliasha hali hiyo kwa kuamua kutoka hapo ulipo na kusonga mbele.

Sijawahi kumuona mtu akichukua kitu cha thamani na kukiweka sehemu ya hovyo hovyo vitu vyote vya thamani hua vinawekwa sehemu ambayo mtu hawezi kuifikia kirahisi. Angalia hata nyumba nzuri lazima iwekewe geti na ukuta mkubwa hii inaonyesha uthamani wa ile nyumba, vitu vyote vya thamani vipo sehemu ambazo haziendeki kirahisi, hivyo usidhani kwamba kuna njia rahisi ya kufikia mafanikio, lazima ukubali kupoteza pesa, kupoteza nguvu, na vitu vingine vingi ili ufikie kile unachokitaka. Kama unachokitaka hakina thamani itakua ni rahisi sana kukipata. Wala huwezi kuumia, huwezi kupitia changamoto kubwa.

Nataka leo utambue  kwamba safari uliyoichagua siyo rahisi na unatakiwa uweke juhudi kubwa Zaidi ii uweze kufika. Ukweli hakuna kisichowezekana ila utashindwa tu pale utakapokubali kushindwa, pale utakapoamua kurudi nyuma, pale utakaposema bora niishi maisha haya ya kawaida tu. Hapo ndio utakua umeshindwa, hakuna njia rahisi kabisa. Unafikiri ni rahisi sana wewe kumeza madawa ya kulevya tumboni ili uyasafirishe upate pesa haraka haraka? Ni rahisi ufanyiwe operation uingiziwe madawa tumboni leo ili kesho uwe tajiri? Ni rahisi kwenda kupambana na polisi wenye silaha kali ili upore mamilioni ya pesa kwa siku moja? Hakuna kitu kirahisi kabisa duniani. Unafikiri ni rahisi sana wewe kubakia katika hali hiyo uliyonayo sasa? Mambo yanabadilika wewe kubakia katika hali uliyonayo ni hatari na ngumu kuliko kuendelea mbele. Kama kuna kitu unakitegemea kwa sasa jaribu kuvuta picha miaka mitano ijayo kitakua wapi. Je bado utakua unaweza kukitegemea kama sasa? Hali ya maisha itakuaje? Hapo utatambua kwamba ni muhimu sana wewe kusonga mbele kuelekea kutimiza ndoto zako.
Inawezekana ukiamua, Amua leo fanya kazi kwa bidi jifunze na ufikie ndoto zako.
Karibu sana
Jacob Mushi
Siri 7 za Kua Hai Leo
0654726668
jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading