Hakuna wa Kukuzuia

Katika zama hizi za Ulimwengu wa Kiteknolojia mambo mengi sana yamerahisishwa mno. Kwa chochote unachokifanya kama kinahitaji kuwafikia watu njia za kuwafikia zimekua rahisi sana.

Kama unatengeneza bidhaa na unataka kuwafikia wateja wengi Zaidi kila kitu unaweza kufanya kwa kupitia kiganja chako.

Kama wewe unaimba huhitaji kwenda kuomba redioni tena wapige nyimbo zako unaweza kuzifikisha moja kwa moja kwa wasikilizaji wako.
Kama wewe unapenda kuigiza kwa sasa huhitaji sana kwenda kwenye Tv uombe ruhusu ya kurusha igizo lako, unaweza kutumia simu yako ya mkononi ukawafikia wale unaotaka wakutazame.

Unaandika huhitaji kwenda kwenye gazeti uombe waandike Makala zako ili zisomwe na watu wengi, kwa kupitia mitandao ya kijamii unaweza kuwafikia watu wengi sana kuliko hata gazeti moja.

Kila kitu unachotaka kukifanya leo kuna njia rahisi Zaidi ya kukikamilisha na kufikia mafanikio. Ni mambo machache sana yatakua yanakuzuia tu. Mambo yenyewe ni kama tabia zako na kutokujifunza.

Amua leo kuchukua hatua kufanya kile unachokitamani na uanze kufikia mafanikio makubwa, kila kitu kimekua rahisi teknolojia imerahisisha mambo ni sisi wenyewe tuweze kuitumia vyema kuifanya dunia sehemu bora ya kuishi.

UFANYE NINI?
Kwanza hakikisha umejua vyema kabisa ni kitu gani unataka kukikamilisha kwenye maisha yako. Yaani hakikisha umejua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani halafu ujue jinsi ya kuanza kuliishi. Kama una kipaji basi hakikisha umefahamu vyema kipaji chako na uanze kukifanyia kazi.

Pili unatakiwa uwe na sehemu yako wewe ambayo utaitumia kuonyesha ule uwezo wako na vyote vilivyopo ndani yako. Vile vinavyofaa kuonyeshwa kupitia mitandao ya kijamii ndio utaanza kuvifanyia kazi. Sehemu hii ni Blog yako ambayo utaweka vile unavyotaka watu wavione au wakujue wewe ni nani na unafanya nini. Kwa kupitia blog unaweza kuwafikia watu wengi sana kuliko unavyofikiri. Bonyeza hapa ujipatie blog 

Kitu cha tatu unatakiwa ujue jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii ili kupata watu wanaofuatilia kile unachokifanya. Kwa kupitia mitandao ya kijamii unaweza kuwafikia wengi mno ambao watakua ni wafuatiliaji wako.

Kitu cha muhimu cha kujua ni kwamba huwezi kumfurahisha kila mtu kwa kile unachokifanya. Kuna watu ambao watapenda unachokifanya na watakufuatilia. Kitu cha kufanya Zaidi ni kujiendeleza Zaidi juu ya kile unachokifanya ili uweze kua bora kila siku.
Hakuna wa kukuzuia wewe ufikie mafanikio dunia inakungoja uanze. Acha kulalamika wakati kila kitu kipo rahisi sana ni wewe kujua ni namna ya kuanza kufikia mafanikio.
Karibu sana.
Success Kingdom
Jacob Mushi
0654726668

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading