“Kinachokupa Matumaini na Kiburi ni hali nzuri uliyonayo sasa hivi”

Bahati mbaya sana unajisahau kwamba unachokitegemea ipo siku kinaweza kuwa na ukomo.

Usisubiri hali iwe mbaya ndipo uanze kutafuta njia nyingine ya kipato,

Usisubiri Mambo Yaharibike ndipo ukumbuke kuchukua hatua, jiandae mapema kwasababu hakuna anaepanga mabaya lakini siku zote tunayaona yakitukuta.

Hali itakapokuwa mbaya ndipo utakumbuka muda uliokuwa unautumia vibaya na watu wasio na maana kwenye Maisha yako.

Sasa hivi una kiburi na una dharau sana kwasababu ya hali nzuri sana uliyonayo, utakuja kukumbuka wale waliokuwa wakikueleza ukweli kwamba unapotea ukawadharau na kuona hawana maana.

Waliokwambia uache anasa ujenge Maisha yako ukawaona ni waganga njaa. Waliojaribu kukuelekeza namna ya kuweka akiba ukawaona hawajui maana ya  msemo wa “tumia pesa ikuzoee”

Hali itakapokuwa mbaya ndipo utakumbuka uzuri ulionao sasa ungefaa kutumika kukuingizia kipato halali na sio kujiuza.

Hali itakapokuwa mbaya ukashindwa kushika ujauzito ndipo utakumbuka idadi kamili ya mimba ulizotoa. Usisubiri hali iwe mbaya ndipo ujute. Hutaweza kubadilisha chochote.

Soma: Uadilifu

Hakuna anaetakiwa ayajali Maisha yako kwa kiasi kikubwa kama wewe mwenyewe, hii ni kwasababu hata wengine wakikujali sana hawana wanachoweza kubadilisha bila ya ruhusa yako.

Usisubiri hali iwe mbaya ndipo uanze kuwa mnyenyekevu na kuongea na watu vizuri. Wakati huu ukiwa na kila kitu ndio wakati bora wa kujiwekea akiba kwa wengine.

Usisubiri hali iwe mbaya ndipo ujitokeze kwenye mambo ya wengine. Wakati huo utakuwa ni aibu na hutothubutu kuwatazama watu machoni.

Wakati unafanya mambo maovu yote kumbuka kuna nyakati zitafika utahitajika kuwa kitu ambacho watu wanajifunzia je watajifunza nini kwako?

HALI ITAKAPOKUWA MBAYA NDIPO UTAKUMBUKA KWENDA KANISANI, KUOMBA USHAURI, KUSOMA VITABU, KWENYE KUSALI. BAHATI MBAYA SANA WAKATI HUO NDIO UTALIPA GHARAMA KUBWA SANA KWASABABU HALI YAKO NI MBAYA.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668,

Twitter: jacobmushitz

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page  

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading