Habari Rafiki, karibu kwenye somo letu la leo ndani ya mtandao huu. Kuna kitu unakwenda kujifunza leo kwenye mtandao huu.

Unajua siku ikishapita imepita lakini kuna kitu kimoja unaweza kuendelea kukosea usipokijua. Ni kweli huwezi kubadili chochote  kwenye Maisha ambayo umeshayaishi bali unaweza kutengeneza Maisha mapya ambayo unayataka tena.
Utakosea sana kama jana itapita bila ya kukupa funzo lolote kwenye Maisha yako. Utaendelea kukosea tena kesho kama hakuna ulichoijifunza kwenye jana yako.
Usikubali kuendelea kufanya makossa yale yale ambayo ulishafanya siku zilizopita. Ukiona hivyo ujue kwamba husongi mbele badala yake unarudi nyuma.
Tengeneza namna ambavyo utaweza kujizuia kurudia makossa ya jana. Kukosea tena kwenye mambo mapya ni ishara kwamba kuna vitu vipya unafanya na unasonga mbele.
Kila hatua unayopiga ina somo kwa ajili ya hatua ya mbele yake. Ukishindwa kutambua somo ulilojifunza utaona huko mbele unakokwenda panakuwa pagumu Zaidi.
Unapaswa kutambua hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya. Ukipata hasara ujue kuna kitu unakumbushwa. Ukitapeliwa kuna kitu unafundishwa, ukiibiwa, ukiumizwa, ukipoteza mali zako kuna somo unafundishwa. Badala ya kulalamika na kusema hali imekuwa ngumu kwako angalia ni kitu gani Mungu anataka ujifunze.
Nikutakie mwaka mpya 2018 wenye baraka na mafanikio kwenye kila unalokwenda kufanya.
Ni mimi Rafiki yako Jacob Mushi.

” Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Simu: 0654 726 668,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading