Hapa Ndipo Unapokosea.

Haiwezekani wewe unatamani kuja kua Mwimbaji bora wa kimataifa halafu muda wako mwingi ukautumia kufuatilia siasa zaidi.

Haiwezekani wewe unatamani kuja kua mfanyabiashara mkubwa halafu muda wako mwingi unafuatilia mpira. Unawajua wachezaji bora kuliko wafanyabiashara bora. Huko ni kupoteza muda tumia muda mwingi zaidi kwenye kile unachotaka kuja kua. Tafuta na fuatilia taarifa nyingi zaidi za kile unachotaka kuja kua. Kama unafuatilia sana Bongo Fleva/Gospel Music nikikuuliza una malengo gani juu ya mziki miaka mitano ijayo uniambie. “Nataka niwe na nyimbo kadhaa” Kama unafuatilia siasa zaidi nikikuuliza una malengo gani juu ya siasa uniambie “2020 nitagombea udiwani” Kama ni biashara uniambie miaka mitano ijayo “natamani niajiri watu 50 kwenye biashara yangu” Kama ni tofauti na hapo huna malengo yeyote juu ya hicho unachokifuatilia zaidi ni bora uache. # Jacob_ Mushi #+255654726668

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *