Mhamasishaji wa Kimataifa Les Brown aliwahi kusema kwamba sio kuwa wtau hawana malengo watu wana malengo lakini ni madogo sana kiasi kwamba wanayatimiza haraka sana bila ya changamoto yeyote.

Unapaswa kuweka malengo makubwa ambayo hata usipoyafikia basi yatakuwa yamekuwezesha ufike mbali sana. Ndoto yako inatakiwa iwe kubwa kiasi kwamba inakuhamasisha kuamka asubuhi na mapema uende ukapambane itimie.

Kule unapokwenda panatakiwa pawe ndio chanzo kikuu cha hamasa yako. Kama kazi yako haikupi hamasa maana yake inaweza kuwa haikulipi au huipendi.

Endelea kushika kukuza maono yako kwasababu una nafasi ya kufikiria vitu vikubwa. Kile unachokifikiria kinawezekana.

Acha kuweka malengo madogo kama kujenga Nyumba, kununua gari, kuoa/kuolewa na uende mbele Zaidi katika kufanya vitu vinavyogusa Maisha ya watu. Weka maono makubwa katika kubadili dunia, kutatua matatizo kwenye jamii inayokuzunguka.

Fanya kile unachokipenda na hakikisha unakifanya hadi kikutengenezee kipato cha uhakika ili uweze kukifurahia Zaidi. Japokuwa mwanzo ni mgumu basi inaakiwa mbele ya mwanzo iwe na matumaini ambayo yanakupa nguvu ya kuendelea mbele Zaidi.

Naamini unaweza kutengeneza Ndoto kubwa ambayo itakufanya ufanye kazi kwa bidii sana ili Ndoto yako ije ikatimie. Chukua maarifa haya ukayafanyie kazi ili uweze kufikia maono yako.

Weka Maono Kwenye

Afya, hapa unapanga vile unavyotaka kuwa kiroho, kiakili na kimwili. Lazima uzijali sehemu hizi za muhimu ili uweze kupata matokeo bora kwenye chochote unachokifanya. Hakikisha unasali na kujifunza kuikuza roho yako yaani umjue sana Mungu, Soma Vitabu kila siku, Fanya mazoezi na hakikisha unakula chakula bora.

Kazi, unataka watu wakutambue kama nani? Kitu gani upo tayari kukifanyia kazi kila siku hadi kikutambulishe? Hapa weka maono makubwa halafu uyafanyie kazi kila siku.

Fedha, weka maono ya kifedha, jua ni kiwango gani cha pesa ukiwa nacho kitaweza kukupa uhuru wa kupata uwezo wa kutatua matatizo yako yote ya kifedha.

Mahusiano, tengeneza mahusiano mazuri na watu, kuanzia mpenzi wako, ndugu zako na jamii inayokuzunguka. Jua unataka watu wakutambue kwa namna gani na ifanyie kazi hiyo. Jua ni mchango gani unataka kuutoa kwenye jamii yako.

Nakutakia Kila La Kheri.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading