Habari za leo rafiki yangu unaendelea vyema na mapambano ya maisha? Leo tunakwenda kujifunza Hatua mbalimbali za kuleta mafanikio katika maisha yetu na hadi kufikia utajiri. Kama tunavyojua kila kitu kinaanza kwa vitendo na kisha vitendo hugeuka kua tabia ukiweza kufanya kwa vitendo mambo haya ya leo utaweza kufikia utajiri. Cha muhimu ni kutambua kwamba wote tunajifunza na tunaelekea huko mimi nakushirikisha nilivyojifunza karibu tujifunze pamoja.

1.  Jijengee Imani ya mafanikio.
Watu wengi tumezaliwa katika maisha na mazingira  ambayo yalitufanya tuamini kwamba hatuwezi kufanikiwa/kua tajiri, sisi ni watu wa chini, watu wa kawaida peke yake, na hivyo tukaendelea kukua na Imani hiyo hadi hapa tulipo. Kitu cha kwanza ni wewe kuanza kufuta Imani mbovu juu ya kumiliki utajiri. Ukijijengea Imani nzuri itakuwezesha wewe kufikia kile unachokitaka. Kumbuka mafanikio ni kila hatua unayoipiga kufikia malengo na ndoto zako.
Hizi ni mojawapo ya Imani za kimaskini unazotakiwa kuziacha:

Watu wenye pesa ni wabaya,
Matajiri wanajijali wenyewe,
Haiwezekani nikawa tajiri,
Sina bahati,
Sina elimu ya kutosha,
Kwetu ni masikini wote,
Pesa haileti furaha,
Pesa ni chanzo cha uovu,
Sio lazima wote tuwe matajiri.

Anza kuamini kwamba inawezekana kufanikiwa kwenye chochote unachokitaka kwenye maisha yako. Futa Imani zote mbovu zilizojengeka kichwani kwako na utaanza kuvutia mafanikio.

2.  Kua na ndoto na malengo.
Kama umeshaweza kujijengea Imani nzuri juu ya utajiri na mafanikio sasa anza kufahamu kile unachokitaka kwa kujua nini unatamani kua nacho kwenye maisha yako. Andika vyote kwenye note book yako. Andika malengo ya kuvifikia hivyo vitu vyote unavyovitaka kama unataka kumiliki nyumba nzuri haiwezi kutokea kwa siku moja au mwaka mmoja. Kwenye ndoto hapa hakikisha chochote unachokiandika umeandika vyema na hadi gharama yake kama ni nyumba hakikisha unaijua thamani yake na pia tarehe siku na mwaka unaotaka kumiliki vitu hivyo. Hii itakusaidia kwenye kuweka malengo vizuri na kuijengea akili yako kuvutia njia nyingi za kupata unachokitaka. Malengo yapo ya muda mrefu na muda mfupi hapa ndipo unapogawanya vile vitu unavyovitaka jinsi ya kuvipata. Kama ni nyumba na umeshajua gharama yake unaweza kuigawanya ile pesa ujue ndani ya mwaka natakiwa kiasi gani  miaka mitano na kadhalika.

3.  Fanya kile unachokipenda/tafuta tatizo kwenye jamii la kutatua.
Malengo na ndoto ulizoziandika ili zitimie lazima uwe na kitu unachokifanya cha kukuingizia pesa. Vitu vya kufanya vipo vingi sana lakini huwezi kufanya kila kitu. Lazima utambue ni kitu gani unapenda kufanya au tatizo gani lipo kwenye jamii inayokuzunguka na unaweza kulitatua na likakuletea pesa hadi ukaweza kutimiza malengo yako. Ukishajua unachokipenda au tatizo la kutatua unatakiwa uwe na maono makubwa juu ya kile unachokifanya. Tuseme labda kwenye ndoto zako zote ili ziweze kutimia unahitaji Tsh milioni 100 yaani ukiwa na milioni mia moja kila unachokitaka kitakua kimetimia. Unatakiwa ujue kwenye kile unachokipenda au tatizo unalotatua utahudumia watu wangapi na watakulipa kiasi gani kutokana na huduma unayoitoa ili baada ya miaka kadhaa (ya malengo yako) uwe umetimiza ndoto na malengo yako. Unaweza kusema huna mtaji mimi nakwambia tafuta namna yeyote unayoweza kuanza bila mtaji mkubwa au bila mtaji kabisa.

4.  Tafuta kiongozi/Kocha.
Huwezi kwenda sehemu usio ijua bila kua na kiongozi, huwezi kufanikiwa vyema kama huna mtu anaekushauri na anaekuongoza kwenye kile unachokifanya. Hivyo nakushauri tafuta mtu ambaye anafanya kile unachokifanya wewe vizuri Zaidi na akafanikiwa ujifunze kwake. Inawezekana asiwe anafanya unachokifanya lakini anaweza pia kukushauri na kukuelekeza kitu cha kufanya ukapata mafanikio. Hauwezi kufanikiwa peke yako unahitaji msaada kwa watu ambao wameshafanikiwa hata kwa ushauri kusoma historia zao za mafanikio, kusoma vitabu vyao.

5.  Fanya kazi kwa bidii usikate tamaa.

Kila kitu ulichokiandika kitakuja kwa kufanya kazi kwa bidii hakuna namna nyingine, jifunze vizuri unachokifanya kama ni biashara ifahamu vya kutosha. Vumilia changamoto zozote unazokutana nazo, wako watakaokwambia huwezi usikate tamaa.

6.  Jifunze kila siku.
Kama umeweza kusoma Makala hii upo kwenye njia nzuri kitu cha muhimu cha kuweza kufikia mafaniko makubwa na utajiri ni kujifunza kila siku hakikisha haipiti siku hujaongeza maarifa kwenye kichwa chako. Unaweza kujisomea kitabu kimoja kila mwezi kama ndio unaanza lakini kama unasoma hakikisha angalau kwa wiki kitabu kimoja. Huwezi kuamini tajiri wa kwanza wa dunia anajifunza kila siku. Siku hizi njia za kujifunza zimerahisishwa sana unaweza kujifunza kupitia simu yako ya mkononi, kuna audio books unasikiliza vitabu vilivyosomwa kujipatia audio books bonyeza Jipatie Audio Books . Kuna magroup ya Whatsapp unayoweza kujifunza. Maarifa yapo kila mahali ni wewe ujue maarifa sahihi kwa kile unachokifanya

7.  Tengeneza tovuti/blog
Kama unafanya biashara yeyote katika ulimwengu wa sasa na inakukutanisha na watu kumiliki tovuti yako ya biashara au hudumu yako ni kitu ambacho hakizuiliki. Unaweza kusema biashara yako bado ni change lakini ukiweza kumiliki blog au tovuti utaweza kuitambulisha biashara yako kitaifa na kwa wafanyabiashara wadogo na wajasiriamali unaweza kuanza na blog ambayo ni bure hulipii chochote.  Bonyeza hapa kutengenezewa Blog. Pia na kurasa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kutambulisha biashara yako hii pia itakuandalia uwanja mkubwa wa kuifikia ile ndoto yako.

Usiogope hakuna kisichowezekana.

Asante kwa kufuatana nami mpaka mwisho.

Karibu tuweze kufanya kazi pamoja kwenye Program inayoitwa WEKEZA ACADEMY Kufahamu Zaidi namna ya kujiunga na WEKEZA ACADEMY Bonyeza Hapa.

Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading