Kwenye safari yetu ya mafanikio kuna vitu vingi tunafanya ili tusonge mbele kila wakati. Ili mtu atoke sehemu moja aliyokuwepo na kusogea mbele anahitaji kulipa gharama.

Sio kitu kirahisi kama unavyoweza kufikiri ndio maana sio wote wanaweza.  Watu wengi huingia kwenye biashara au huanza vitu vipya na kutegemea matokeo bila kulipia gharama yeyote.

Kama ilivyo kwa Mtoto anavyozaliwa ili aweze kupitia hatua za ukuaji anahitaji kulishwa chakula bora na vilevile matunzo ya kutosha. Haiwezekani mtoto akizaliwa leo aachwe hovyo hovyo halafu tutegemee akue kirahisi lazima ataugua na mwishoe kufariki.

Hivyo pia kwenye vitu tunavyofanya tunahitaji uvumilivu,  kujifunza, kufanya kazi kwa bidii, muda wa kusubiri matokeo.

Haitokei tu ghafla ukaanza kuona matunda ya mti. Lazima zipite hatua mbalimbali hadi uone matunda. Hata unapootesha nyanya ukaziacha shambani bila kuzihudumia usitegemee mabadiliko yeyote. Zaidi utakuta zimeharibika.

Kabla jambo lolote linapotokea kwenye maisha yako. Iwe ni biashara imekufa au kuna kitu umeanza halafu hujaona matokeo usilalamike na kuchukia wale waliokuonyesha jiulize umelipia gharama?

Ulitoa muda wako kuvumilia?  Ulijifunza vya kutosha?  Maana hakuna matokeo yanayotokea hivi hivi.

Ili kupiga hatua yeyote ya kimaisha Unahitaji kulipa Gharama. Kuna watu hufikiri ukishasoma Kitabu kilichoandikwa siri za mafanikio baada ya hapo utafanikiwa. Ukweli ni kwamba ili upate mafanikio lazima uzifanyie kazi zile siri.

Asante sana.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 | 0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading