Kila kinachotokea Maishano mwako kinatokea Kwasababu.  Changamoto yeyote unayopitia ipo Kwasababu. Ugumu wa Maisha unaopitia upo Kwasababu. Ukosefu wa pesa ulionao upo Kwasababu.

Kuachwa na umpendae imetokea Kwasababu. Kudharauliwa kumetokea Kwasababu. Kusemwa kunatokea Kwasababu.
Hakuna kinachotokea kwa Bahati mbaya hata siku moja. Kuna sababu nyuma ya lolote linalotokea. Umefanikiwa Kwasababu ulifanya kazi kwa bidii.
Badala ya kulalamika au kumtafuta wa kumlaumu kwenye changamoto unayopitia jiulize ni sababu imesababisha.
Kama ni fursa imekupita sababu ni hukujiandaa vyema. Cha kufanya ni kujiandaa ili wakati Mwingine usipitwe.
Inawezekana umeachwa sababu ni uzembe wako wewe mwenyewe. Inawezekana pia ni Mungu anakuandalia Bora zaidi.
Sikwambii utafute sababu za kujitetea la hasha!  Nataka ufahamu sababu ya tatizo linaloendelea kwako sasa hivi ili urekebishe lisijitokeze tena.
Kama mpaka sasa hujaanza biashara Kwasababu ya kukosa mtaji huo ni ujinga. Na hiyo sio sababu. Ni Ukweli huo jaribu kuangalia namna nyingine ya kuzungumza. Rafiki Yangu na Kocha Amani Makirita anasema mwaka 2017 sababu hiyo usithubutu kuingia nayo Yaani mwaka 2017 tafuta sababu nyingine ya kujitetea kwanini hujaanza biashara lakini isiwe hii ya kukosa mtaji.  Na mimi nakazia hapo kwa kukwambia huo ni ujinga kukosa mtaji ni kushindwa kufikiri.
CHA KUFANYA: Ijue sababu inayosababisha tatizo ulilonalo na usiishie kuijua tu. Tafuta suluhisho la sababu hiyo ili utoke hapo ulipo uende HATUA nyingine.
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com ,  www.jacobmushi.com

jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading