HATUA YA 100: Ukweli na Uwazi

jacobmushi
By jacobmushi
2 Min Read
Siku zote kama wewe ni mwongo huwezi kuwa muwazi utakua unadanganya vitu vingi. Katika Maisha yetu kila siku kuna mambo ambayo yanahitajika kusemwa na mengine yanabaki kama siri ndani ya mioyo yetu.
Katika mambo ambayo yanahitajika kusema ili uweze kuwa huru ni vyema sana ukawa msemakweli. Iwe ni kwenye biashara yako au huduma yeyote unayotoa kuwa mkweli. Iwe ni kwenye familia kuwa mkweli.
Imekuwa ni tabia ya wafanyabiashara wengi kuwaahidi mambo mbalimbali wateja wao lakini hawatekelezi kwa wakati. Unapokuwa muwazi unamfanya mtu awe na uwanja mpana wa kufanya maamuzi.
Unapodanganya unajiweka kwenye nafasi ya kudanganya tena. Unajitengenezea mazingira ya kutokuaminika.
Hua napenda kusema mfano kwenye mahusiano. Wewe leo unasema hutaki mwenzi wako ashike simu yako ni sawa kwasababu kuna mambo unadhani hatakiwi kujua. Lakini unatakiwa ujue kwamba ipo siku utakuwa mgonjwa huwezi kushika simu itabidi ishikwe na wengine hayo unayoyaficha yatajificha yenyewe?
Soma: Kitu gani Kinakutambulisha?
Ipo siku utapoteza simu itaokotwa na uovu uliokuwa unafanya utaonekana pia. Badala ya kufanya maamuzi ya kumzuia mtu ashike simu yako jaribu kuwa mwadilifu. Kuwa mwadilifu kwasababu ndio Maisha uliyoamua kuishi. Utaishi Maisha ambayo hayana wasiwasi.
Kuna wakati unaweza kupata tatizo ambalo litawalazimisha wengine wapekue simu yako ili upate utatuzi sasa kama una tabia mbovu mbovu zitakuja kujulikana.
Ukweli na uwazi unakuja tu pale mtu anapokuwa mwadilifu kwenye biashara yake, kwenye mahusiano na Maisha kwa ujumla.
Usikubali kuishi Maisha ya hofu na wasiwasi kwasababu ya tabia mbovu ulizonazo kuwa mwadilifu na utaishi Maisha ya uhuru sana.
Tabia zako halisi ni zile unazopenda kufanya bila kujulikana, hizi nyingine unazoonyesha mbele za watu ni maigizo tu.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading