HATUA YA 104: Nyuma ya Pazia

By | March 28, 2017
Jambo lolote zuri unaloliona kwa nje kuna watu walihusika katika kulifanya liwe zuri. Watu hawa mara nyingi wanaweza wasionekane au wasiwe maarufu kama jambo lenyewe lakini ndio wanafaidika Zaidi.

Watu wengi wanapenda kuonekana mbele za watu lakini hawataki kukaa chini na watu wawatengeneze. Lazima ukubali utengenezwe nyuma ya pazia kabla hujajitokeza mbele ukiwa bora.
Vitu vyote vizuri unavyotamani kuja kuvimiliki kabla hujaenda mbali sana hakikisha basi na wewe kuna watu kadhaa wanatamani kuwa na kitu ulichokitengeneza wewe. Unatamani kwenda sehemu moja nzuri sana kuliko zote hapa duniani, ili uweze kufika jitahidi japo kidogo kuwe kuna vitu vyako wewe wengine wanavitumia au kuvimiliki.
Nyuma ya pazia ndiko kunakopikwa vitu badala ya wewe kutamani vitu vizuri sana halafu huwezi kuwa navyo kwa sasa chagua kuwa nyuma ya pazia. Ukishakuwa nyuma ya pazia anza kutengeneza  vitu ambavyo watu wataanza kuvitafuta.
Usitamani sana wewe uanze kuonekana sana kabla ya bidhaa yako. Bidhaa yako ndio ionekane kwanza halafu watu watatafuta wenyewe mmiliki wa bidhaa. Tatizo linakuja pale wewe unataka kuwa maarufu kuliko bidhaa yako.

Kaa nyuma ya pazia hadi watu waje wakutafute huko. Kaa nyuma ya pazia pika vitu hadi watu watakuja kukutoa wenyewe uje ushuhudie. Usiwe na haraka sana utafahamika tu iache bidhaa yako ijulikane kwanza.

Upo tayari kukaa nyuma ya pazia? Huu ni mtihani mgumu sana kwa wengine maana tumejengewa tabia ya kutaka kujionyesha mbele za watu. Wengi tunavaa mavazi ya gharama simu za ghali ili watu watuone. Kitu cha ajabu ni kwamba wamiliki wa hivyo vitu tunavyovaa hata hawajulikani.

Unapoona filamu imekuwa bora na maarufu sana kuna watu walikaa nyuma ya pazia wakatengeneza. Watengenezaji hawawi maarufu kama waigizaji hivyo usitamani kuwa maarufu kuliko bidhaa yako.
Kaa Nyuma ya Pazia tengeneza Bidhaa.
Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *