Unafurahia kufanya vitu gani? Unajua kuna yofauti ya kufurahia kufanya vitu na kupenda kufanya vitu Fulani?

Mtu anaweza kufurahia sana kulala hasa wakati wa asubuhi lakini anajua kabisa ni hatari kwa mafanikio yake.
Mtu anaweza kufurahia kufuatilia habari zisizomhusu wala kumsaidia lakini anajua kabisa anapoteza muda. Halafu mtu huyo huyo ukimwambia kuhusu kusoma vitabu atakwambia hana muda.
 Mtu anaweza kufurahia kukaa na makundi mabovu  baa au kijiweni akidai anabadilishana mawazo lakini hata siku moja hayupo na watu wanaofanya kazi.
Mtu anaweza kufurahia kula vyakula vya hovyo lakini anasahau kwamba vinamletea magonjwa na mwili mbovu. Mtu huyo huyo anachukia magonjwa sana.
Mtu anaweza kufurahia kuishi Maisha yasiyo na  mazoezi mwili wake ukawa hauko imara sana na akashambuliwa na magonjwa haraka sana.
Vitu vingi sana unavyovifurahia kufanya mara nyingi havina faida kubwa sana ya baadae. Vina faida ya muda huo huo lakini madhara ni ya baadae. Kuna vile vitu ukivifanya kama vile vinaumiza sana lakini kwa baadae vinaleta faida kubwa sana.
Jitazame mwenyewe na ujifanyie tathmini je vitu unavyofurahia kufanya sasa vina matokeo gani kwa baadae? Unafurahia kuangalia filamu sasa hivi kwa masaa kadhaa kila siku unategemea matokeo gani huko baadae?
Jifanyie tathimini na uanze kubadilisha vitu ambavyo vinaleta furaha muda huo huo lakini matokeo mabaya baadae.
Unafurahia kufanya ngono zembe sasa hivi lakini baada ya muda utapata magonjwa au mimba zisizotarajiwa.
Amua kubadilika sasa anza kuishi Maisha yale ambayo yanaleta matokeo bora huko baadae.
Kuna mtu mmoja akaniambia kwamba usipofanya vitu Fulani huko baadae hutapata muda wa kuvifanya. Nikamwambia kama hivyo vitu havina faida kwenye hayo Maisha ya baadae basi hakuna haja ya kutumia muda mwingi kwenye vitu hivyo.
Jiunge na Semina Kwa njia ya mtandao. Muda ni mchache umebaki semina inaanza tarehe 15/4/2017 fanya malipo mapema ada ni tsh elfu tano tu. Mawasiliano ni 0654726668
Jipatie nakala yako ya kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo piga 0654726668.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading