Mara nyingi biashara inapokuwa inaanza inaakua na njia nyingi sana na nzuri za kumjali mteja. Ila kadiri inavyokuwa na kupata wateja wengi huanza kushuka taratibu kwenye kuwajli wateja na ubora wa huduma.

Kama na wewe umeingia kwenye kundi hili upo hatarini kuua biashara yako mwenyewe. Hatari inakuja Zaidi pale kile unachokifanya wako wengine wanakifanya pia. Ukishindwa kutumia mbinu mbalimbali za kumfanya mteja apende kuwa kwenye biashara yako atahama.
Kwanza hakikisha unatoa huduma nzuri na bora kwa wateja wako. Wakati mwingine mtu hanunui kwasababu ya bidhaa nzuri peke bali hata kwa namna anavyohudumiwa. Ukiweza kumhudumia vyema akajisikia yupo sehemu salama lazima atafika kila wakati.
Huduma kwa wateja ni sehemu pana sana ambayo unatakiwa ujifunze kulingana na aina ya biashara yako ilivyo.
Kitu cha pili ni kuhakikisha thamani ya bidhaa inaendana na thamani ya pesa inayouzwa. Sio kitu unauza elfu kumi halafu kina thamani ya elfu tano. Mteja akiona hivyo lazima akimbie. Hakikisha mteja wako anapotumia bidhaa yako aone inaendana au ni Zaidi ya pesa aliyolipia.
Kama bidhaa itakuwa ipo chini na pesa ipo juu wateja wataona unawaibia. Na hakuna mtu ambaye yupo tayari kuibiwa. Watu wanatafuta pesa zao kwa shida halafu wewe unataka kuja kuzichukua kirahisi tu. Thamani ya bidhaa inaweza isiwe kwenye bidhaa ndani yake pekee inaweza kuwa namna ambavyo unaitoa hiyo bidhaa, ndio maana unaweza kukuta bei za maji ya kunywa au soda zinatofautiana kulingana na mazingira.
Hakikisha mambo mawili ya muhimu sana kwenye biashara yako unayazingatia. 
Karibu sana
Your Partner in Success 
Jacob Mushi 
Entrepreneur & Author 
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418 
Email:
jacob@jacobmushi.com  
Blogs:
www.jacobmushi.com,  www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading