Habari ya leo ndugu yangu mpendwa. Ninamshukuru kwa kufika hii hatua ya 108 bila ya kuacha kuandika hata siku moja. Nafurahi na wewe kuendelea kuwa msomaji wangu wa kila siku. Ninaamini kabisa kuna vitu unavipata hapa na vinakusaidia sana kwenye Maisha yako. Tuendelee pamoja hadi tufikie mafanikio makubwa sana. Kila sehemu unayoifanyia kazi hakikisha hauishii kuwa mtu wa kawaida.

Leo ni tarehe 1 mwezi wa nne. Tumemaliza robo ya mwaka sasa yaani ni miezi mitatu imepita tangu tuanze mwaka huu 2017. Ni habari njema sana hizi kwani tunapata nafasi ya kuangalia tulipoanzia na tulipofika vilevile tunapokwenda. Wakati ndio unatakiwa ujitazame je ni kweli unasonga mbele? Je kweli bado upo kwenye njia au umeshaacha njia unaelekea porini?
Siku ya leo tafuta muda wa kutosha kabisa uyatazame yale uliyosema unakwenda kuyatekeleza ndani ya mwaka huu. Je ni kweli umeanza japo kuona mwangaza?
Mambo mengi tunayofanya yanahusiana na watu hivyo ili malengo ya wengi yatimie inategemea ni kwa jinsi gani watu wanaitikia kile unachokifanya. Kwa namna moja au nyingine watu wanaweza kuwa changamoto kwetu kwasababu hawatabiriki. Unaweza kuweka malengo kesho unataka uuze kiasi kadhaa kwenye biashara yako lakini hilo litatokea tu pale watu watakapoamua kununua kwenye biashara yako. Wewe hauhusiki moja kwa moja kuzitoa pesa mfukoni kwa watu bali kwa kuongea maneno ya ushawishi.


Vilevile watu wengine wanaweza kuwa changamoto na kukurudisha nyuma ni wale ambao unategemea wafanye majukumu Fulani halafu hawakutekeleza kama wewe ulivyowaagiza au ulivyokuwa unatarajia. Haya ni mambo ya muhimu sana kuzingatia katika Maisha ili uweze kujua kuzibeba changamoto vyema. Mfano ni pale umepanga kukutana na mtu saa saba kamili ukajitahidi kabisa wewe ukafika saa saba kasoro lakini yeye akafika saa nane kasoro au asije kabisa.
Haijalishi umefikia wapi au ni kwa kiasi gani changamoto hizo unapitia bado unayonafasi ya kurekebisha. Na wakati huu unaoendelea ni wa muhimu sana ili makosa yaliyojitokeza kwenye miezi hii mitatu yasijirudie tena huko tunakokwenda.
Hakikisha umeainisha chini changamoto zote zilizokukwamisha kwenye hatua ulizokuwa unapiga. Hakikisha unapata suluhisho lake kabla hatujaendelea kusonga mbele. Kadiri unavyoacha viporo vingi ndio mambo yanazidi kuwa mazito huko mbele. Na hii itapelekea sababu ya kushindwa kukamilisha malengo yako.
Karibu sana ndugu yangu.
Kama mpaka sasa hujamiliki Blog unaachwa mbali sana badili mtazamo wa biashara yako hapa…
Jiunge na Semina ya itakayofanyika kwa Njia ya Mtandao hapa…..
Jipatie Vitabu Uongeze Ufahamu wako Hapa…..
Karibu sana.
Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading