Maisha yako yanazidi kuwa magumu sana kutokana na mizigo mingi uliyobeba. Kuna mizigo mingine haina umuhimu wowote kwenye Maisha yako. Wakati mwingine Maisha yako yanaweza kuwa magumu kwasababu ya mizigo mingi uliyoibeba kwenye akili yako na katika uhalisia.
Marafiki wabaya.
Hawa wanaweza kuwa mizigo mikubwa kwenye Maisha yako kama utashindwa kuwawekea mipaka. Marafiki hawa wanaweza kuwa sababu kubwa ya wewe kurudi nyuma kwenye yale unayoyafanya. Usikubali Maisha yako yaendeshwe na marafiki hawa. Tunaposema marafiki wabaya unaweza usielewe ni watu wa aina gani.
Marafiki wabaya ni wote wale wasioleta mchango chanya kwenye Maisha yako. Ni wote wale ambao hawawezi kukushauri juu ya kutafuta pesa ila wanajua kutumia Zaidi. Kama marafiki zako mara nyingi mnakutana kwenye kutumia Zaidi kuliko kwenye kuzalisha hao ni marafiki mizigo. Marafiki ambao wakikutana na vitu vizuri vya kufanya hawakushirikishi kabisa wanafanya wakishaafaidika ndio wanakuja kukuuliza na kushangaa kwanini hukujua hao pia ni mizigo. Rafiki wa kweli hawezi kukutana na kitu kizuri akakaa kimya asikwambie.
Kununua vitu usivyovitumia.
Hii ni aina ya mzigo ambao unawatesa watu wengi sana kwenye Maisha hasa kipindi hiki. Unakuta mtu akiwa na pesa mfukoni atanunua kila kizuri kinachomvutia mbele yake. Kama na wewe una utumwa huu ukimbie mara moja kwa Maisha yako yatazidi kuwa magumu Zaidi. Unaweza kujikuta unanunua vitu vingi unavijaza ndani lakini hujawahi kuvitumia. Kaa chini sasa tazama ni vitu kiasi gani umejikuta unanunua na huna matumizi navyo.
Unaweza kuja kushangaa pesa zinakwenda wapi, mbona ukipata pesa haikai kumbe wewe una tabia hii ya kununua kila kinachokuvutia. Unapokwenda dukani muuzaji kazi yake ni kukufanya wewe ununue hivyo atatumia ushawishi wa aina yeyote ununue kile ulichokiangalia. Kama unajijua una tabia hii ni bora usitembee na pesa nyingi au ukipata pesa usiendee maeneo ya masoko.
Jiiunge na semina itakayofanyika kwa njia ya mtandao kujifunza Zaidi bonyeza hapa
Jipatie kitabu cha Siri 7 za kuwa hai leo, piga 0654726668
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com, www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.