Furaha yako inatoka wapi? Nataka ujiulize leo furaha yako inatokana na nini!  Kila mmoja ana jibu lake juu ya chanzo cha furaha yake.

Kama furaha yako inaletwa na vitu au watu kuna wakati utakosa furaha. Wakati vitu havipo utakosa furaha, watu wakikuacha utakosa furaha.
Kama furaha yako inaletwa na mali nyingi utaishi bila furaha hadi ufikie hizo mali nyingi lakini mwisho wa siku utajikuta hujaishi kabisa.
Kamwe Usikubali kuweka chanzo cha furaha yako katika vitu au watu. Usiweke furaha  yako katika vitu vya kuharibika.  Chanzo cha furaha yako kinatakiwa kitoke ndani yako.
Kama ilivyo kwa mtoto mdogo ndivyo unavyotakiwa kuishi. Mtoto ambaye hajatambua vitu hua anakuwa na furaha wakati wote.
Kinachotuharibu sisi na kutuondolea furaha zetu ni kwa kujilinganisha na wengine. Ukimuona mwenzako ana vitu bora na vingi kuliko wewe unasononeka. Unasahau hata kile ulichonacho.
Furaha isiletwe kwako kwa wingi wa mali au vitu. Furaha isiletwe kwako na mtu Mwingine zaidi yako mwenyewe. Furahia maisha wakati huu unapoishi. Furahia na kile kidogo unachopata. Hakuna kitu kingine cha kukuongeza furaha ila ni wewe mwenyewe.
Karibu sana. 

Jacob Mushi 
Entrepreneur & Author 
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418 
Email: jacob@jacobmushi.com 
Blogs: www.jacobmushi.com , www.jacobmushi.com  
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading