Habari Rafiki, leo tena tunatazama baadhi ya mizigo mingine ambayo inaweza kuwa sababu yaw ewe kushindwa kusogea mbele.  Yapo mambo mengi sana yanatusonga kwenye Maisha lakini kiukweli hayana umuhimu wowote kwani yanazidi kuturudisha nyuma.

Mambo Yaliyopita.
Mambo mbalimbali yaliyokwishapita kwenye Maisha yetu yanaweza kuwa mizigo mizito sana ambayo inatufanya tushindwe kusonga mbele. Inawezekana ulipitia mambo mabaya na magumu sana hadi unajikuta kila wakati unawaza na kujiona huna bahati, au una mikosi. Lakini ukweli kama jambo limeshapita kama hakuna cha kujifunza achana nalo mara moja.
Mambo yaliyopita yanaweza kuwa mizigo mikubwa sana hasa tunapoyakumbuka wakati tunafanya mambo ya wakati huu. Dawa pekee ya kukuwezesha wewe uachane na mambo yaliyopita ni kwa kuyasahau na kutumia muda mwingi Zaidi kushughulika na kule unapoelekea.
Chuki/WIvu/Visasi
Kama moyoni mwako utabeba chuki kwa ajili ya waliokufanyia mabaya utashindwa kufanya mambo mengine. Wasamehe kwani huwezi kufuta yale waliyokufanyia. Haijalishi una vidonda vikubwa kiasi gani wasamehe.

Wivu nao ni mzigo badala ya wewe kuridhika na kile ulichokipata huku ukiongeza bidi unaonea wivu vya wengine. Wivu huwa chanzo cha chuki na baadae utafikiwa kutaka kuharibu wengine ili wewe upate.
Visasi ni vibaya sana vinakufanya ushindwe kufurahia safari yako ya mafanikio. Visasi vinakufanya uwaze juu ya maadui zako mara zote. Wasamehe na ondoa yote ndani ya moyo.
Unatakiwa utumie muda na nguvu nyingi juu ya maono yako. Achana na waliokuumiza.
Kujifunza Zaidi Jiunge na Semina itakayoendeshwa online Bonyeza Hapa Kujiunga..

Jipatie Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo Wasiliana nami kwa 0654726668

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading