Msukumo kwenye kile unachokifanya unaletwa na nini? Msukumo kwa yule unaesema unampenda unasababishwa na nini?

Ukiweza kuniambia msukumo huo unasababishwa na kitu gani naweza kukwambia utafika mbali kiasi gani na hicho unachokifanya au huyo ulienae.
Kama wewe unasukumwa na pesa, yaani kilichokuvutia Zaidi kwenye fursa Fulani ni kwasababu ulisikia kuna pesa sana usipoziona pesa utaacha.
Nilikuwa nafanya biashara ya Mtandao na kampuni Fulani watu wengi niliokutana nao wanasema sababu kubwa ya wao kushindwa au kuacha biashara ni kwamba waliambiwa kuna pesa lakini hawajaziona.
Msukumo wako kwenye kitu ulichoamua kukifanya hadi ufikie hatua Fulani kubwa inatakiwa usiwe ni wa vitu vinvyoweza kupotea au ambavyo ukivikosa utashindwa kuendelea.

Mara nyingi nakutana na watu wengi wananiuliza mimi ninafaidika nini kupitia kuandika kila siku. Jibu moja ambalo napenda kuwajibu ni kwamba msukumo wangu mkubwa unatokana na kile kilichopo ndani yangu. Natamani kuona jamii iliyobadilika kifikra na inayofanya yale mambo yanayopaswa kufanyika na sio kufuata tamaa zao.
Wewe kama mfanyabiashara au mjasiriamali shauku yako kubwa ni ipi? Je ni umaarufu? Je ni kupata fedha nyingi?
Jiulize ukifanya hicho unachokifanya sasa hivi na ukakosa umaarufu utaendelea kukifanya? Ukafanya hicho unachokifanya na usipate utajiri uliokuwa unautamani sana je utaendelea kufanya?
Sio vibaya kabisa kutamani utajiri au kuwa maarufu sana lakini kama unafanya vitu ili upate vitu hivyo utajikuta unateseka sana na kuwa mtumwa wa kila kinachokuja mbele yako maana unachokitaka hakitakuja kwa haraka.
 Endelea kufanya kazi kwa bidii bila lengo la biashara yako iwe ni kutatua matatizo ya jamii fedha na umaarufu vitakuja pale utakapotatua matatizo ya wengi. Utakapogusa Maisha ya wengi watu wataanza kuzungumza habari zako. Utakapogusa Maisha ya wengi fedha zitaanza kukukimbilia kwenye biashara yako.

Jiunge na Semina Itakayoendeshwaa Online Hapa

Jipatie Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai Leo nipigie 0654726668
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading