Wakati mwingine huwa tunatamani sana kusikia wengine wanatuambiaje, wengine wanasemaje juu ya kile tunachofanya ili kupata hamasa Zaidi. Lakini kabla ya yote lazima wewe mwenyewe uanze kujikubali kutoka ndani.

 

Kama wewe mwenyewe utajikataa na kujiona huwezi hakuna atakaeweza kuja kukusifia. Ili uweze kufanya mambo makubwa Zaidi lazima kwanza uanze kujikubali kutoka ndani.
Kabla hujapongezwa anza kujipongeza, kabla watu hawajasema utakuja kufanikiwa anza kujiona wewe mwenyewe ni mtu wa maafanikio makubwa.

 “The person you see is the person you will be. Create a positive self-image for yourself.”

Yule mtu unaemwona ndani yako ndio wewe utakuja kuwa. Tengeneza picha chanya na nzuri sana kwa ajili yako. Anza sasa kujisemesha maneno mazuri. Anza sasa kujinenea mafanikio. Anza kujiona ukiwa kwenye nafasi ya juu.
Katika Maisha haya ya sasa unaweza kusubiri sana watu waanze kukwambia maneno mazuri lakini usipate anza mwenyewe.
Kuna wakati unakosea lakini makosa yasiwe sababu ya wewe kupoteza ile picha nzuri ndani yako. Tambua makosa yako lakini endelea kujiona unaweza kufanya vizuri Zaidi.
Unatakiwa utambue kuna wakati utafanya jambo zuri sana na asitokee hata mtu mmoja wa kukupongeza. Kama utakuwa una tabia ya kujikubali wewe mwenyewe jambo kama hilo halitakupa shida yeyote.
Kuna wakati utafikia hatua ambayo utajiona upo mwenyewe hakuna alie karibu yako, hakuna anaekutia moyo. Kama hujajijengea tabia ya kujitia moyo mwenyewe utakuwa kwenye wakati mgumu sana.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading